Kwa Mara ya Kwanza Wataalamu Wazawa Wazibua Mishipa Pacha ya Moyo Iliyoziba kwa Asilimia 95
Apr 11, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Wataalamu wazawa wa magonjwa ya moyo na wazibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimzibua mgonjwa mishipa miwili iliyokuwa inapeleka damu kwa wakati mmoja kwenye moyo iliyokuwa imeziba kwa asilimia 95 na kupata shida ya kupitisha damu. Uzibuaji wa mishipa hiyo ulifanyika kwa njia ya upasuaji wa moyo kwa kutumia tundu dogo bila kufungua kifua kwa kutoboa mshipa kwenye paja kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambayo ni maabara inayotumia mionzi maalum kwa ajili ya uchunguzi na tiba za magonjwa ya moyo.