Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga
Sep 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_14478" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (mbele) leo akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi (hayupo pichani) aliyekuwa akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga, lililoanza leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.[/caption] [caption id="attachment_14479" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini, Bi. Malika Berak mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere katika Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga lililoanza leo.[/caption] [caption id="attachment_14482" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wananchi waliotembelea meza ya maonesho ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayokwenda sambamba na Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga linalofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.[/caption] [caption id="attachment_14485" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prosper Tesha (kulia) akiwa na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Prof. Zacharia Magnilwa (katikati), wakimsikiliza Mhandisi Kedrick Chawe, kwenye maonesho yanayokwenda sambamba na Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafiri wa Anga yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.[/caption] [caption id="attachment_14488" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai nyekundu aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Usafiri wa Anga linalofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kushoto kwa Waziri ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi na kulia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Bw. Hamza Johari.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi