Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kiswahili Chapaa Kikanda na Kimataifa, Kuazimishwa katika Kila Balozi za Tanzania Duniani
Jun 06, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki - WUSM


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa lugha ya Kiswahili inaendelea kupata heshima ulimwenguni  baada ya kutengewa siku yake duniani ya Julai 07 kila mwaka ambapo uamuzi huo wa kihistoria umeipaisha vyema lugha hiyo.


Akiwasilisha  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2022/23, Mhe. Mchengerwa amesema kuwa, wizara kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) inaendelea na mkakati wa kuongoza Dunia kuadhimisha siku hiyo hapa nchini na katika Balozi zote za Tanzania duniani.


"Katika kipindi hiki naweza kujinasibu kuwa, matumizi ya Kiswahili yanazidi kukubalika kitaifa, kikanda na  kimataifa ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/22 zimezaa matunda kwa kiswahili kuvishwa joho jipya kwa kuwa lugha ya kazi Umoja wa Afrika", amesema Mhe. Mchengerwa.


Ameongeza kuwa baadhi ya Vyuo Vikuu vya Nje ya Tanzania ambavyo awali havikua na Programu za kiswahili vimeanza harakati za kuingiza kiswahili katika programu zao ambapo tayari kuna makubaliano ya awali ya kushirikiana kati ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Ethiopia, Chuo Kikuu Cha Port Harcourt (Nigeria) na Chuo Kikuu Joachim Chisano (Msumbiji) katika kufundisha kiswahili.


Katika mwaka ujao wa 2022/23, wizara itaendelea kuwekeza katika lugha hiyo, ikiwemo mafunzo, kuongeza idadi ya wakalimani, kufundisha wanafunzi wengi zaidi ili lugha hiyo iendelee kukua zaidi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi