Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kiswahili Chaendelea Kupata Sifa Kimataifa
Feb 14, 2026
Kiswahili Chaendelea Kupata Sifa Kimataifa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa katika Maadhimisho ya miaka 10 ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA), yaliyoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Zanzibar
Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali  Ndg. Gerson Msigwa amesema Lugha ya Kiswahili imeendelea kukua na kupata sifa kimataifa kutokana na kuongezeka kwa watumiaji.

Msigwa amesema hayo wakati akimuwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Paul Makonda katika Maadhimisho ya miaka 10 ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA)  yaliyofanyika Februari 14, 2026 Zanzibar yaliyoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Lengo la maadhimisho hayo ni kuimarisha maendeleo na matumizi ya Kiswahili ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika na Dunia kwa ujumla. Aidha, yanakusudia kukuza Kiswahili kama lugha ya mawasiliano, biashara na utamaduni pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kikanda kupitia lugha hiyo.

          

          
Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya dhamira ya kuimarisha maendeleo ya Kiswahili ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, yakionesha wazi kuwa Kiswahili si tu chombo cha mawasiliano bali pia urithi hai wa utamaduni, mshikamano na maendeleo ya watu wa ukanda huu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi