Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kero za Muungano Zinakaribia Kumalizika
Mar 26, 2024
Kero za Muungano Zinakaribia Kumalizika
Waziri wa Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Na Ahmed Sagaff - Maelezo

Takriban kero nne zilizobakia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaofikisha miaka 60 zinaendelea kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema jitihada za kutatua kero hizo zimeimarika katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Jafo amezitaja kero hizo kuwa ni mgawanyo wa mapato yatokanayo na hisa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki.

Nyingine ni mgawanyo wa faida kutoka Benki Kuu na uingizwaji wa sukari inayozalishwa katika kiwanda cha Mahonda katika soko la Tanzania Bara.

"Ufanisi umekuwa mkubwa sana. Nilitoa takwimu hapo mwanzo kwamba kipindi hiki tumeweza kutatua takribani kero 15 za Muungano. Hili si jambo dogo kwa kipindi cha miaka mitatu kuweza kufanikisha," amearifu Dkt. Jafo.

Naye, Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Mobhare Matinyi amefahamisha kuwa Watanzania wanajivunia historia ya Taifa lao katika miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano ulioasisiwa Aprili 26, 1994.

"Natoa wito kwa Waandishi wa Habari na kuwaomba ushirikiano wenu katika kipindi hiki cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano," ameomba Ndg. Matinyi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi