Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Afanya Kikao na Watumishi Wake, Asisitiza Suala la Kuhamia Mji wa Serikali
Apr 03, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41657" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza na wafanyakazi wa Wizara yake Aprili 02, 2019 Jijini Dodoma kuhusu kuboresha utendaji kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.[/caption]

Na Shamimu Nyaki -WHUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi amesema kuwa  ujenzi wa  Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali  Mtumba Jijini Dodoma  zipo katika hatua za mwisho  kukamilika na kuwataka watumishi wake kuwa tayari  kuhamia kati ya mwezi wa nne na wa tano mwaka 2019.

 Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma wakati  wa kikao na Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilicho wapa  fursa  wafanyakazi hao kiliwakutanisha   fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali ya kiutendaji.

“Ni vyema mkajiandaa na kuwa tayari  kuhamia mji wa Serikali kwakua kwa sasa ofisi zipo katika hatua za mwisho kukamilika na matarijio yangu ni kwamba kati ya mwezi wanne na wa tano tutakuwa tumehamia rasmi”.alisema Bibi.Susan.

[caption id="attachment_41654" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi (kushoto) akizungumza katika Kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Susan Mlawi (kulia) na Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichokua na lengo la kuimarisha utendaji kazi kilichofanyika April 02,2019Jijini Dodoma.[/caption]

Aliongeza kwa kueleza kuwa  Wizara imefanya michakato mbalimbali ya kuhakikisha inawakwamua watumishi wake kiuchumi kwa kuanzisha  SACCOS pamoja na Mfuko wa kufarijiana wenye lengo la kuwasaidia watumishi katika masuala mbalimbali ya kijamii .

Aidha  Katibu Mkuu huyo amewataka  watumishi  kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo ili kuleta matokeo chanya katika utendaji, huku akisisitiza kuwa hakuna haki bila wajibu.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bw. Orest Mushi amewataka watumishi hao kufuata na kuzingatia sheria , taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma katika utendaji wa kazi.

[caption id="attachment_41656" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akitoa maoni katika Kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi (hayupo pichani) na Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichokua na lengo la kuimarisha utendaji kazi kilichofanyika April 02,2019Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_41655" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifuatilia Kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi (hayupo katika picha) kilichokua na lengo la kuimarisha utendaji kazi kilichofanyika April 02, 2019.[/caption]      

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi