Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu Watembelea Idara ya Habari
Nov 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Nicholous William wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi baada ya kuwasili katika ofisi za Idara hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Idara hiyo kujionea utendaji kazi wake mapema leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nicholaus William.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Susan Mlawi (katikati) akisoma Jarida la NCHI YETU linalotolewa na Idara ya Habari (MAELEZO) alipofanya ziara katika Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Nicholaus William na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholous William (kulia) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi walipotembelea Ofisi za Idara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Suzan Mlawi, Jarida maalum la NCHI YETU linaloelezea miaka miwili ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano. 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholous William Mlawi, Jarida maalum la NCHI YETU linaloelezea miaka miwili ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano. 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi