Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Kampuni ya Zechy Africa Yaja na Chemichemi Carnival
Jul 26, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_7516" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa tamasha la Chemichemi Carnival Bi. Lena Kimani akisisitiza juu ya tamasha litakalofanyika tarehe 9 na 10 mwezi Septemba 2017 katika kijiji cha Makumbusho wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Zechy Africa, Bi. Dorah Raymond na Mkurugenzi wa Operesheni wa Kampuni ya Zechy Africa Bw. Ally Nchahaga (kushoto).[/caption]

Na. Thobias Robert 

Kampuni ya Zechy Africa inayojihusisha na masoko imeandaa tamasha kwa ajili ya kusherehekea  utamaduni wa Mtanzania linalotarajiwa kufanyika mapema mwanzoni mwa mwezi wa tisa katika Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa tamasha hilo Bi. Lena Kimani alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Tamasha hilo linaloitwa Chemichemi Carnival na kusisitiza kuwa tamasha hilo litafanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 9 -10 mwaka huu.

  [caption id="attachment_7519" align="aligncenter" width="640"] Waandishi wa habari wakimsikiliza Mratibu wa Tamasha la Chemichemi Carnival Bi. Lena Kimani wakati akizungumza nao juu ya Tamasha la Chemichemi Carnival katika ukumbi wa Idara ya Habari - Maelezo.[/caption] “Tumeendaa tamasha hili la Chemichemi Carnival kwa lengo la kuonesha utamaduni halisi wa Mtanzania, wananchi watumie fursa hii kujitokeza kwa wingi kuja kujionea tamaduni mbalimbali za kitanzania,” alisema Bi. Lena. Aidha Bi. Lena aliongeza kuwa utamaduni wa Mtanzania unazidi kupotea hasa kwa vijana wanaozaliwa na kukulia Mijini hivyo tamasha hilo litaendeleza na kukuza utamaduni wa Mtanzania ili vijana wasisahau tamaduni zao. “Kutokana na utandawazi na mwenendo wa maisha Watanzania wanaoishi mijini wengi wao hawana ukaribu na vijiji wanakotoka na hili limewafanya vijana wengi wa sasa kuwa mtazamo hasi kuhusu utamaduni ,” alieleza Bi. Lena. Tamasha hilo linatarajia kuonesha mambo mbalimbali ya kiutamaduni likijumuisha, maonesho ya mavazi, vyakula, burudani kutoka ngoma za asili, wadau mbalimbali wa sanaa pamoja na mashindano ya mitindo kwa washiriki.   [caption id="attachment_7520" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Operesheni wa Kampuni ya Zechy Africa Bw. Ally Nchahaga akifafanua jambo kuhusu tamasha la Chemichemi Carnival litakalofanyika tarehe 9 na10 Septemba 2017 katika kijiji cha Makumbusho wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Zechy Africa, Bi. Dorah Raymond na Mratibu wa tamasha la Chemichemi Carnival Bi. Lena Kimani. (Na: Mpiga Picha Wetu)[/caption]

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Dorah Raymond amesema kuwa Tamasha hilo linatarajia kuwakutanisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi ili kukuza fursa ya kiuchumi kupitia sanaa na tamaduni zitakazooneshwa katika tamasha hilo.

 Alisema kuwa tamasha la hilo linaleta watu wote pamoja katika kusherehekea tamaduni zetu lakini pia fursa za kukua kiuchumi kupitia sanaa.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Zechy Africa Bw. Ally Nchahaga ameongeza kuwa kufuatia umuhimu wa kukuza utamaduni wa mtanzania tamasha la Chemichemi Carnival litakuwa likifanyika mara mbili kwa mwaka.

“Tamasha hilo ambalo litafayika kwa mara ya kwanza hapa nchini, halitakuwa na kiingilio, badala yake wananchi wahamasishwa kujitokeza kwa wingi wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ili kuongeza hamasa,” aliongeza Ally Nchahaga

Kampuni ya Zechy Africa imeandaa Tamasha hilo ikiwa ni mara ya kwanza kwa tamasha hilo kufanyika hapa nchini ambapo kupitia kampuni hiyo litakuwa likifanyika kila baada ya miezi sita ili kutoa fursa kwa tamaduni mbalimbali kushiriki katika tamasha hilo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi