Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JWTZ Kuandaa Mkutano Mkuu Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani
Feb 20, 2024
JWTZ Kuandaa Mkutano Mkuu Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), Meja Jenerali Francis Ronald Mbindi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
Na Ahmed Sagaff - Maelezo

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) limeteuliwa kuandaa Mkutano Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani unaotarajiwa kufanyika Mei 13-17, 2024 jijini Dar es Salam.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), Meja Jenerali Francis Ronald Mbindi amesema mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe 300 kutoka nchi 140 ulimwenguni.

"Mgeni rasmi siku ya ufunguzi Mei 13, 2024 anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na siku ya kufunga Mei 17, 2024 mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa," ameeleza Meja Jenerali Mbindi.

Naye, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Michezo JWTZ, Kanali Martin Msumari amesema katika kipindi cha mkutano huo kutakuwa na michezo ya kipaumbile ambayo ni pamoja riadha na mchezo wa ngumi.

JWTZ ilijiunga na Baraza hilo mwaka 1973 na tangu ilipojiunga imepata fursa ya kuandaa mkutano huo mwaka 1991 na 2024 huku amani iliyopo Tanzania ikitajwa kuwa kivutio kikubwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi