[caption id="attachment_50642" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi, Zena Ahmed Said, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50641" align="aligncenter" width="750"] Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Nishati na Wizara ya Ardhi, Makamishina wa Jeshi la Magereza na Zima moto na Viongozi wengina wa Serikali wakiwa katika hafla ya kuapishwa kwao Ikulu Jijini Dar es Salaam, baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli.[/caption]
Na Eric Msuya
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi walioapishwa kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za uongozi pamoja na kuwa na hofu ya Mungu bila kusahau kutanguliza Uzalendo katika kuhakikisha Tanzania inafikia malengo iliyojiwekea.
Rais Magufuli Ameyasema hayo leo tarehe 3 Februari 2020 katika hafla ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
“niwapongeze sana kwa majukumu yenu mapya ambayo nina amini mtakwenda kuyafanyia kazi kwa Uzalendo wa Kweli na bila Kusahau Kumtanguliza Mungu na kufanya kazi kwa kufuata sheria katika utendaji kazi wenu huko mnapoenda” amesema Rais Magufuli
[caption id="attachment_50643" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Prof. Riziki Shemdoe, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50644" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Christopher Kadilo katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption]Sambamba na hilo Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kwa utendaji kazi wake katika kuisemea Serikali.
“Dkt. Abbasi umefanya kazi nzuri sana kwa kuisemea vizuri Serikali, nakupongeza sana kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu hivyo utaendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali hii mpaka atakapopatikana mtu mwingine “ amesema Rais Magufuli
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amemshukuru Rais Magufuli kwa kujaza safu na kuteua Viongozi katika mahakama hivyo kwenda kurahisisha upatikanaji wa huduma.
[caption id="attachment_50646" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50647" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, akisaini kiapo mara baada ya kula kiapo hicho katika katika hafla ya kuwaapisha viongozi walioteuliwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimpa vitendea kazi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020. [caption id="attachment_50649" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimvisha Cheo kipya Kamishina wa Jeshi la Magereza, Brigedia Jenerali, Suleiman Mzee, kabla ya kumuapisha katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption]“Nashukuru Rais magufuli kwa kuendelea kujaza safu za mahakama, umetupatia viongozi ambao wana weledi wa kazi hii ya mahakama, hivyo nina amini kabisa tunaenda kufanya kazi a kuwatumikia watanzania” amesema Jaji Mkuu
Miongoni mwa walioapishwa leo na Rais Magufuli ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wizara ya Nishati, Bi Zena Ahmed Said, katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Christopher Kadilo, Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Bi Marry Gaspar Makondo.
Wengine walioapishwa leo na Rais Magufuli ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Steven Mhoja Mashauri, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza
[caption id="attachment_50650" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimvisha Kofia Kamishina wa Jeshi la Magereza, Brigedia Jenerali, Suleiman Mzee, mara baada ya kumuapisha katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50651" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimvisha Cheo kipya Kamishina wa Jeshi la Zima moto, DCP John Wiliam Masunga, kabla ya kumuapisha katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50652" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akimuapisha Kamishina wa Jeshi la Zima moto, katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateuwa hivi karibuni iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50653" align="aligncenter" width="750"] Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Nishati, Wizara ya Mmabo ya Ndani na Wizara ya Ardhi, pamoja na Makamishina wa Jeshi la Magereza na Zima moto na Viongozi wengina wa Serikali wakila kiapo cha Maadili, katika hafla ya kuapishwa kwao Ikulu Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_50656" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kulia waliokaa) na Jaji Mkuu Ibrahimu Jumaa ( kushoto waliokaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, TAMISEMI, Nishati, Katiba na Sheria, Mambo ya Ndani, Viwanda, Habari pamoja na viongozi walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50657" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, (Watatu kulia) akisaini kiapo cha Maadili mara baada ya kula kiapo hicho katika hafla ya kuapishwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption] [caption id="attachment_50655" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akisisitiza jambo kwa viongozi wa Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali mara baada ya kuwaapisha Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.[/caption]Emmanuel Mpawe Kukube, Naibu katibu Mkuu wizara ya nishati Leonard Robert Masanya.
Kwa upande kwa Mahakama Viongozi walioapishwa ni Msajili Mkuu wa mahakama ya Tanzania Wilbert Chuma, Msajili wa Mahakama ya Rufani Kelvin David, pamoja na Kamishna wa Magereza Brigedia Jenerali Suleiman Mzee na Kamishna wa Jeshi la zima moto na uokoaji John Wiliam.