Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Yang'ara Kimataifa Upasuaji wa Moyo kwa Watoto
Jul 05, 2018
Na Msemaji Mkuu

Katika kuimarisha uhusiano na uboreshaji wa upasuaji wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo kwa watoto Tanzania kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imechaguliwa kuwa kituo cha ufuatiliaji na shirika la (International Quality Improvement Collaborative for Congenital  Heart Surgery (IQIC) la nchini Marekani.

Kabla ya kuchagulia kuwa kituo cha mafunzo mwaka jana mwezi wa 12  Shirika la IQIC ambalo linasimamiwa na Hospitali ya kimataifa ya watoto ya Boston nchini Marekani  liliangalia Hospitali ambayo inafanya kazi  zake vizuri katika upasuaji wa moyo kwa watoto na kuomba taarifa ya kazi walizozifanya kwa kipindi cha  miaka miwili iliyopita.

Kutambulika kwake kimataifa na kuwa moja ya vituo 66 kutoka nchi 25 Duniani Taasisi yetu itatumika kutoa elimu katika nchi za Afrika, wataalamu kutoka IQIC watakuja kutoa elimu kwa madaktari wetu pamoja na madaktari wengine wa moyo kwa watoto  wa Afrika.

Kwa upande wa watoto kliniki yetu  kila siku inatoa huduma kwa  wagonjwa 25 hadi 30 na kulaza mgonjwa mmoja hadi wawili . Mwaka jana upasuaji wa kufungua kifua ulifanyika   kwa watoto 182 na bila kufungua kifua kwa watoto 92.  Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2018 jumla ya watoto 82 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua  watoto 26.

Zaidi ya asilimia 75 ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na magonjwa yanayoshambulia milango  ya mishipa mikubwa na midogo ya moyo. Asilimia 25 ni wale ambao walizaliwa salama lakini wameyapata matatizo hayo baada ya kuzaliwa.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Kupitia kipimo hiki  mtoto akigundulika kuwa  na tatizo la moyo ataweza kupatiwa  matibabu kwa wakati  na hivyo kuwa na afya njema kama watoto wengine.

Imetolewa na:

Kitengo cha Uhusiano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

04/07/2018

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi