Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imedhamiria kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa kufungua kliniki mbili mpya za matibabu ya moyo zilizopo Kawe katika jengo la Mkapa Health Plaza na nyingine katika jengo la Osterbay Plaza.
"Huduma tunazotoa ni uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto na watu wazima, kliniki za mishipa ya damu, huduma za maabara, mazoezi tiba, huduma ya matibabu majumbani,elimu ya afya, lishe bora na mafunzo kwa jamii.
Huduma nyingine ni pamoja na matibabu ya magonjwa ya ndani, duka la dawa, tiba mtandao,huduma ya gari la wagonjwa na huduma ya upimaji wa afya kwa vikundi mbalimbali.
Sanjari na hayo, Dkt. Kisenge amesema kuwa Taasisi hiyo ina mikataba na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Madaktari wa Upasuaji Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika katika kutoa mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo kwa wataalamu wa afya, Chuo Kikuu cha Jagiellonian cha Poland na Chuo Kikuu cha New York cha Marekani kwa ajili ya kufanya utafiti,elimu na utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa moyo.