Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Yaelekea Nchini Zambia Kuweka Kambi Upasuaji wa Moyo kwa Watoto
Jan 17, 2024
JKCI Yaelekea Nchini Zambia Kuweka Kambi Upasuaji wa Moyo kwa Watoto
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule akizungumza na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere kabla ya kuanza safari yao ya kwenda katika hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel ndilo lililowezesha kufanyika kwa kambi hiyo ya upasuaji nchini Zambia.
Na Mwandishi Wetu

Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya wataalamu hao kuanza safari ya kuelekea katika hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel ndilo lililowezesha kufanyika kwa kambi hiyo ya upasuaji nchini Zambia.
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt. Gen. Mathew Edward Mkingule akiagana na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Angela Muhozya mara baada ya kuwaaga wataalamu wa Taasisi hiyo waliokwenda nchini Zambia kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel ndilo lililowezesha kufanyika kwa kambi hiyo ya upasuaji nchini Zambia.
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia na wataalamu wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto itakayofanyika katika hospitali hiyo kwa muda wa siku tatu. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel ndilo lililowezesha kufanyika kwa kambi hiyo ya upasuaji nchini Zambia.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi