Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JKCI Kushirikiana na Misri Kuboresha Matibabu ya Moyo Nchini
Feb 02, 2024
JKCI Kushirikiana na Misri Kuboresha Matibabu ya Moyo Nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wadau kutoka Kampuni ya STERI CARE iliyopo nchini Misri walipofika JKCI jana kwa ajili ya kuangalia maeneo ambayo taasisi hiyo itashirikiana na kampuni hiyo kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba na ujuzi katika kutoa huduma za matibabu ya moyo.
Na Mwandishi Maalumu – JKCI

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na kampuni ya STERI CARE iliyopo nchini Misri imejipanga kurahisisha upatikanaji wa vifaa tiba vya matibabu ya magonjwa ya moyo nchini.

Ushirikiano huo utagusa eneo la vifaa tiba vya moyo, mavazi yanayotumiwa na wataalamu wa afya eneo la kazi pamoja na kushirikiana katika kubadilishana ujuzi wa kutoa huduma za matibabu ya moyo.

Akizungumza wakati wa kikao na wadau kutoka kampuni ya STERI CARE Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI inatamani kuagiza vifaa tiba kutoka nje ya nchi moja kwa moja ili kupunguza gharama za vifaa itakayopelekea kupungua kwa gharama za matibabu.

“Kama JKCI itapata makampuni makubwa nje ya nchi na kuchukua mahitaji yake huko, gharama za vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya matibabu ya moyo zitapungua lakini pia kupunguza athari za ukosefu wa vifaa hivyo kwa wakati”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge alisema Taasisi itafanya utafiti yakinifu na kuainisha viwanda mbalimbali vinavyotengeneza vifaa tiba ili iweze kufanya navyo kazi kwani uhitaji wa vifaa tiba umekuwa mkubwa.

Naye mwakilishi kutoka kampuni ya STERI CARE iliyopo nchini Misri, Mohmad Tohan alisema kampuni hiyo ipo tayari kufanya kazi na JKCI kwani huduma nyingi zinazotolewa na kampuni hiyo zipo JKCI.

“Leo tumekuja na mavazi ya wataalamu wa afya tuliyonayo ili muweze kuona kazi zetu lakini pia tunavyo vifaa vinavyotumika katika matibabu ya magonjwa ya moyo ambavyo tunaamini mkichukua kwetu gharama zitapungua”, alisema Mohmad

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi