Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jitokekezeni Kusaidia Tasnia ya Sanaa: Naibu Waziri Mhe. Shonza
Oct 24, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_20971" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (aliyesimama katikati) akishuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ametoa wito kwa Kampuni na Taasisi mbalimbali nchini kujitokeza kusaidia tasnia ya sanaa ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini makubailiano ya mradi wa utambuzi wa sanaa za ufundi na uchoraji (TACIP),mkataba uliosainiwa baina ya Kampuni ya Data Vision International na Shirikisho la sanaa za ufundi na uchoraji (Tafca).

[caption id="attachment_20972" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiongea na wadau wa Sanaa na Ufundi wakati wa Hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Naibu Waziri Shonza amesema kuwa mradi huo wa TACIP utasaidia kuwaletea maendeleo wasanii husika kwa kuwa watakuwa wanatambulika kisheria hivyo itakuwa rahisi kwao kupata fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Mradi huu utawezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya kazi za sanaa kwani utawaleta wasanii wote pamoja, ambapo wataweza kujadiliana na kutatuaa kero zao kwa pamoja” alisema Mhe. Shonza.

Aidha Mhe. Shonza alitumia fursa hiyo kuwaponge wabia wote wa mradi huo kwa ubunifu mkubwa waliouonyesha nakuwataka wasanii wa fani zingine waige mfano huo.

[caption id="attachment_20973" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sanaa za ufundi pamoja watendaji wa Kampuni ya Data Vision International mara baada ya kukamilisha Hafla ya Utiaji Saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA) na Kampuni ya Data Vision International 24 Oktoba, 2017 Jijini Dar es Salaam.(Picha Zote na Benedict Liwenga-WHUSM)[/caption]

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi na Uchoraji Tanzania (Tafca) Adrian Nyangamale amesema kuwa mradi huu wa utambuzi wa sanaa za ufundi na uchiraji umekuja wakati muafaka jambo litakalosaidia kulete maendeleo katika tasnia hiyo.

Amesema kuwa lengo kubwa la kubuni mradi huo ni kuhakikisha kuna kuwa na kanzi data ya wasanii wote wa sanaa za ufundi na uchoraji nchini ili waweze kutambuliwa na mamlaka husika.

Naye Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Data Vision International William Kihula amesema kuwa kutokana na ukweli kuwa Kampuni yao inajihusisha na masula la ya ukusanyaji wa takwimu,utoaji wa vitambulisho wameona watoe mchango wao kwa tasnii ya sanaa kama jitihada zao za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano iliyoahidi kupitia Ilani ya uchaguzi kuinua wasainii.

Aliongeza kuwa Data Vision watahakikisha mradi huu wa Jitambue,Tambulika, Inalipa unafanikiwa kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau ambao ni wasanii wa sanaa za ufundi na uchoraji.

Data Vision ni Kampuni inayijishugulisha na masuala ya ICT, UTAFITI, Vitanmmbulisho ambapo limekuwa likifanya kazi kwa karibu zaidi na Serikali kwa takribani miaka 20 sasa limeamua kugeukia sekta zisizo rasmi ili kuweza kutoa mchango wake.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi