[caption id="attachment_42218" align="aligncenter" width="1000"] Meneja wa Usalama Barabarani toka Shirika la Afya Duniani (WHO), Bibi. Mary Kessy akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption]
Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kupunguza ajali za barabarani kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani zinazofanywa na wadau wa usalama barabarani.
Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Deus Sokoni alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendeea kutoa elimu kwa umma pamoja na uboreshaji wa miundombinu ili kupunguza ajali na vifo kwa watanzania.
[caption id="attachment_42219" align="aligncenter" width="1000"] Mwenyekiti wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu usalama Barabarani, Jonas Kamaleki akiongoza majadaliano wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption] [caption id="attachment_42220" align="aligncenter" width="1000"] : Mratibu wa Mafunzo ya Usalama Barabarani kwa Waandishi wa Habari toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Said Makora akielezea jambo wakati wa mafunzo kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption]Mrakibu Msaidizi wa huyo wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Sokoni alisema “Barabara nyingi zinazojengwa hivi karibuni zimekuwa zikizingatia viwango vya ubora vyenye kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa barabara ikiwemo watembea kwa miguu”
Alifafanua zaidi kuwa siku za nyuma barabara hazikuwa zikijengwa kwa ubora wa kuzingatia watumiaji wote wa barabara mfano wa barabara ya Dar es salaam iliyopo jijini Dodoma, ambayo imesababisha ajali mara kadhaa.
Aidha, Mrakibu Msaidizi huyo wa Polisi ametaja jitihada nyingine za Serikali za kupunguza ajali ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko na mchepuko ambazo zinasaidia kuondoa msongamano wa foleni katika majiji mbalimbali nchini.
[caption id="attachment_42221" align="aligncenter" width="1000"] Mkufunzi wa mafunzo ya kuhusu usalama Barabarani, Allan Lawa akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption] [caption id="attachment_42222" align="aligncenter" width="1000"] Mrakibu Msaidizi wa Polisi Trafiki Makao Makuu, Deus Sokoni akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption] [caption id="attachment_42223" align="aligncenter" width="750"] Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Helmet Vaccine Initiative Tanzania, Alpherio Nchimbi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption] [caption id="attachment_42224" align="aligncenter" width="1000"] Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg, Henry Bantu akichangia hoja wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu namna ya kuripoti habari kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption] [caption id="attachment_42227" align="aligncenter" width="1000"] Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Trafiki Makao Makuu, Deus Sokoni akitoa maelekezo kwa waandishi wa Habari kuhusu namna alama za barabarani zinavyotumika wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa Waandishi wa Habari kuhusu usalama Barabarana leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[/caption] [caption id="attachment_42228" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya washiriki wa mafunzo kuhusu usalama Barabarani kwa Wandishi wa Habari wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO). (Picha na: Idara ya Habari -MAELEZO)[/caption]Baadhi ya miradi ya Serikali inayoendelea kutekelezwa kwa lengo la kupunguza ajali na foleni nchini ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko ndani ya Dodoma yenye urefu wa kilomita 39 pamoja na barabara za mchepuko zinazojengwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Naye, Mwendesha pikipiki wa jijini Dodoma Amos Majenda alisema kuwa Serikali imesaidia kupunguza ajali kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani ambayo inawafikia watumiaji wengi wa barabara.
Majenda alisema “Serikali imejitahidi kutoa elimu si kama kipindi cha nyumba ambapo ajali zilikuwa nyingi zaidi, ajali zinazotokea hivi sasa ni kwa sababu watu hawazingatii sheria za usalama barabarani na hivyo madereva wanaendesha vyombo vya moto kwa mwendokasi na kutovaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria”
Mafunzo hayo yanayotolewa kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani nchini yana lengo la kuwajengea uwezo waaandishi wa habari ili waweze kusaidia kufikisha elimu kwa umma, sambamba na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kutatua changamoto za ajali za barabarani nchini.