[caption id="attachment_16294" align="aligncenter" width="1000"] Walemavu wa uziwi wakiandamana kuelekea katika viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro kuadhimisha kilele cha wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa jana Mkoani Morogoro[/caption]
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ifikie muda watanzania tuamue kuifanya lugha ya alama kuwa Kiswahili cha pili ili lugha hii ya alama ijulikane kwa wote na kuunganisha jamii moja na nyingine.
Waziri Mwakyembe ameitoa rai hiyo Jana Mjini Morogoro aliposhiriki Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi duniani ambayo mwaka huu kitaifa yameadhimishwa Mkoani Morogoro katika viwanja vya shule ya sekondari Morogoro na kubeba kauli mbiu isemayo “Ushiriki kamilifu kwa lugha ya alama”.
[caption id="attachment_16297" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza mlemavu wa uziwi (kulia) alipotembelea bidhaa zinazotengenezwa na mlemavu huyo jana Mkoani Morogoro wakati wa kuadhimisha kilele cha wiki ya viziwi duniani.[/caption] [caption id="attachment_16298" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akinunua moja ya bidhaa iliyotengenezwa na mlemavu wa uziwi (kulia) alipotembelea bidhaa zinazotengenezwa na mlemavu huyo jana Mkoani Morogoro wakati wa kuadhimisha kilele cha wiki ya viziwi duniani.[/caption] [caption id="attachment_16299" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa jana Mkoani Morogoro.[/caption]“Serikali inatambua kuwa viziwi wana haki ya kutumia lugha ya alama kama njia kuu ya mawasiliano na jamii inayowazunguka ili kuiwezesha jamii ya viziwi kuongeza wigo na fursa za maendeleo miongoni mwao” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuhakikisha kuwa haki ya kupewa taarifa inatekelezwa ndani ya kipindi cha kwanza kwa utaratibu mzuri uliofanyiwa kazi vizuri ili kuwa endelevu.
Akizungumza kwa kutumia lugha ya alama wakati wa maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Bw. Nidroisi Mlawa ameipongeza serikali kwa kupokea changamoto za viziwi na kuzitatua ndani ya kipindi cha muda mfupi kwani kwa kufanya hivyo viziwi watapata fursa ya kupata taarifa mbalimbali zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi.
[caption id="attachment_16300" align="aligncenter" width="1000"] Wanafunzi wenye ulemavu wa uziwi kutoka shule ya msingi MontFort Morogoro wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa jana Mkoani Morogoro.[/caption] [caption id="attachment_16301" align="aligncenter" width="1000"] Kikundi cha ngoma cha viziwi kutoka mlandizi kikicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa jana Mkoani Morogoro.[/caption] [caption id="attachment_16306" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimkabidhi cheti cha ushiriki Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Stella Ikupa Alex wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa jana Mkoani Morogoro[/caption] [caption id="attachment_16307" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye T-shirt nyeupe waliosimama) katika picha ya pamoja na walemlavu wa uziwi kutoka Mkoani Mbeya wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa jana Mkoani Morogoro. (Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM)[/caption]Kwa upande wake Mwenyekiti Bodi ya CHAVITA Morogoro Bibi. Lucy Nkya ameiomba serikali kuingiza mtaala wa lugha ya alama katika kada mbalimbali kama vile polisi, afya na kada nyingine muhimu ili kuwawezesha maafisa wa kada hizo kupata taarifa ya kweli kutoka kwa viziwi kuliko kupata taarifa kutoka kwa mtu anayetafsiri ambaye wakati mwingine anaweza kufanya hujuma wakati wa kutafsiri hivyo kumkosesha kiziwi kupata haki anayostahili.
Naye Mlezi wa CHAVITA na Mjumbe wa bodi ya CHAVITA Askofu Alex Malasussa ameiomba jamii kuwa na mawasiliano kamili kwa kujifunza lugha ya alama ili kuweza kuishi na watu wenye ulemavu wa uziwi bila kuwanyanyapaa au kuwasema kwani nao wanahitaji kupata taarifa ya mambo yanayoendelea duniani.
Maadhimisho ya siku ya Viziwi duniani ni moja kati ya jitihada za Baraza la umoja wa Mataifa kuhakikisha kuwa fursa mbalimbali za maendeleo za walemavu zinapatikana kwa kushirikiana na jamii inayowazunguka.