Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

IGP Sirro Afanya Ukaguzi Kituo cha Mabasi Ubungo
Aug 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8202" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na madereva wa mabasi ya abiria pamoja na abiria wanaosubiri usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi Luis.[/caption]

Na. Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  amewataka madereva  na wamiliki wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na wamiliki na madereva wa mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala kuhakikisha wanafanya  ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara katika magari yao ili kupunguza ajali zinazosababishwa na ubovu na uchakavu wa magari.

Hayo yamesemwa jana na IGP Sirro wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza  katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja  na kituo cha daladala cha Mbezi  Luisi  kwa lengo la kuangalia hali ya usalama wa kituo hicho,  kuona namna ukaguzi wa mabasi  ya abiria ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali  za abiria.

“Nimefarijika kuona watendaji wa kituo hiki pamoja na askari wangu wakifanya kazi vizuri kwa ushirikiano mkubwa hali inayosaidia kupunguza kero mbalimbali kwa watumiaji wa kituo hiki”  alisema IGP Sirro

  [caption id="attachment_8203" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimuelekeza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Fortunatus Muslim kuhakikisha kuwa magari na mabasi yote ya abiria yanakaguliwa mara kwa mara. IGP Sirro alifanya ukaguzi wa kushtukiza jana katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo na Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis.[/caption] [caption id="attachment_8204" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ( katika) akiwa katika ukaguzi wa kushtukiza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi ( DCP) Lucas Mkondya akifuatiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Haji.[/caption] [caption id="attachment_8205" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro (katika) alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi, (kushoto) ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Murilo Jumanne Murilo.(Picha zote na Jeshi la Polisi)[/caption]

 Aliongeza kuwa Ubungo ni salama na itaendelea kuwa salama  kwa sababu vibaka wamepungua na wale wanaofanya utapeli katika kituo hicho waache mara moja na kutafuta kazi nyingine kwa kuwa mwisho wa siku wataacha familia zao baada ya kukumbana na mkono wa sheria.

Vilevile, IGP Sirro ameelekeza magari yote ya abiria yabandikwe namba simu zote za makamanda wa mikoa wa Kikosi cha Usalama barabarani pamoja na Wakuu wa Polisi wa wilaya zote katika ili abiria waweze kutoa taarifa  pindi wanapoona dereva anaendesha gari kwa kukiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.

Aidha, amewataka  wananchi  kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu, ikiwa ni pamoja kutii sheria bila shuruti  na kutoa wito kwa  wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria kufuata na kuheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka makosa na ajali za barabarani.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi