Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Huduma za Kibenki Kusogezwa Ndani ya Mahakama Jumuishi Mbeya
Aug 30, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34614" align="aligncenter" width="750"] Viongozi wa Mahakama Kanda ya Mbeya (kushoto) wakiwa katika majadiliano na Viongozi wa Benki ya NMB, majadiliano juu ya uanzishwaji wa huduma za kibenki ili kuwarahishia wateja wanaofika katika Mahakama hiyo.[/caption]

Na Rajabu Singana

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba amekutana na uongozi wa benki ya NMB na kufanya mazungumzo juu ya uanzishwaji wa huduma za Kibenki katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya linalotoa huduma kwa Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya.

 Mhe. Makaramba alikutana na uongozi huo mapema Agosti 28, aliwaeleza viongozi wa NMB kwamba Mahakama ipo katika maboresho makubwa ya huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano (2015-2020) unaolenga kumsogezea mwananchi huduma.

Kutokana na changamoto ya kufanya malipo ambayo wamekuwa wakiipata wananchi Mhe. Makaramba aliwaomba NMB kusogeza huduma zao katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya.

Akichangia katika mazungumzo hayo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,       Bw. Straton Chilongola alisema kwa sasa Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Mawakala ambao hufanya kazi za Kibenki.

Bw. Chilongola aliongeza kwa kusema kwamba watafanya utaratibu wa kuanzisha ‘Cash Collection Point’ kwa ajili ya wananchi kufanya malipo ya Huduma za Mahakama.

Meneja wa Wakala wa Benki wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Respicious Denis aliongeza kuwa kwa sasa benki ya NMB imekuwa ikifanya vizuri kwa kutumia Mawakala kwenye malipo na makusanyo mbalimbali ambapo tayari baadhi ya taasisi za serikali zinatumia huduma hiyo. Alizitaja taasisi hizo ni paoja na TRA, Idara ya Maji Mbeya na walitumia mfumo huo katika makusanyo ya NaneNane mwaka huu.

Ifahamike kwamba baada ya ukarabati mkubwa wa jengo la Mahakama Kuu Mbeya, Uongozi wa Mahakama ya Tanzania ulifikia maamuzi ya kulifanya jengo hii kuwa Kituo Jumuishi cha kutoa huduma za Mahakama.

Wadau muhimu wa Mahakama walipatiwa ofisi za kuendeshea shughuli zao ikiwa ni njia mojawapo ya kumsogezea mwananchi huduma na kuondoa usumbufu kwa wananchi. Wadau walipotiwa ofisi ni pamoja na Mawakili wa Kujitegemea, Mawakili wa Serikali, Polisi na Huduma kwa Jamii.

Pamoja na mambo mengine viongozi hawa wameafikiana kuanzisha Huduma za Kibenki wiki ijayo kwa kumtumia Wakala wa Benki.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi