Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

HOTUBA YA WAZIRI WA MADINI, MHESHIMIWA ANGELLAH JASMINE MBELWA KAIRUKI (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA WA 2018/19
May 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

  UTANGULIZI

  1. 1.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kufuatia Taarifa iliyowasilishwa leo Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea, kujadili, na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu, Mpango na Bajeti ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18. Aidha, ninaomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19.
 
  1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi  wa  rehema,  kwa  kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena. Aidha, ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Hotuba ya Bajeti ya Wizara yangu kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19.
 
  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, ninakushukuru kwa kunipa fursa hii adhimu ya kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu kwa mara ya kwanza Bajeti ya Wizara ya  Madini.  Kama  unavyofahamu  Wizara
  hii iliundwa mwezi Oktoba, 2017 baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, na hivyo kufanya bajeti hii kuwa ndiyo ya kwanza ya Wizara mpya ya Madini. Wizara ya Madini inategemea sana mawazo, ushauri na maelekezo ya Bunge lako Tukufu ili kuimarisha na kukuza Wizara hii mpya.  
  1. Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniteua kuwa Waziri wa Madini; Wizara ambayo ni muhimu kwa uchumi wa Nchi yetu pamoja na Manaibu wangu, Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo (Mb.), na Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko (Mb.). Tunamuahidi tutatekeleza maelekezo anayoyatoa kwa ufanisi na uadilifu na tutatekeleza majukumu  yetu  vyema  na  tutatumia ujuzi na maarifa yote tuliyopewa na Mwenyezi Mungu na tuliyojifunza kusimamia Sekta hii ipasavyo ili Taifa letu linufaike na rasilimali za madini.
 
  1. 5. Mheshimiwa Spika, napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa uongozi wake makini katika usimamizi wa rasilimali za nchi. Sote ni mashahidi wa jinsi uongozi wake unavyogusa wananchi wa Tanzania hususan katika matumizi sahihi ya rasilimali za Taifa katika kuwaletea maendeleo.
 
  1. Mheshimiwa Spika, pia ninawashukuru Makamu wa Rais, Mheshimiwa  Samia  Suluhu  Hassan  na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwa miongozo wanayonipatia katika kutekeleza majukumu yangu kikamilifu.
 
  1. Mheshimiwa Spika, katika  suala  hili  la usimamizi wa rasilimali za nchi na hususan katika Sekta ya Madini ninayoisimamia, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Rais na wewe binafsi kwa kuunda Kamati ambazo zilishughulikia changamoto zilizopo katika Sekta ya Madini. Mapendekezo ya Kamati zote yamefanyiwa kazi na baadhi ya mapendekezo mengine yanaendelea kutekelezwa. Nawahakikishia kuwa, Wizara yangu itatekeleza mapendekezo yote kama yalivyotolewa na Kamati hizo.
 
  1. 8. Mheshimiwa Spika, vilevile, nikupongeze wewe binafsi, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb.), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb.), na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha Bunge kwa weledi mkubwa, hekima, busara na kwa umahiri.
 
  1. Mheshimiwa Spika, ninachukua fursa hii pia kuwashukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula (Mb.), Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mariam Ditopile Mzuzuri (Mb.) na Wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kwa michango yao  mahsusi  wakati  wa  uchambuzi wa Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 na Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19. Kamati imetoa maoni mbalimbali na ushauri mzuri unaoboresha utekelezaji wa majukumu yetu na kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha Taifa. Napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa Wizara ya Madini itafanya kazi  kwa karibu na Kamati hii kwa manufaa na maslahi ya Taifa.
 
  1. 10. Mheshimiwa Spika, sina  budi  kuwashukuru kwa dhati Viongozi wenzangu wa Wizara ya Madini Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo (Mb.), Naibu Waziri, Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko (Mb.), Naibu Waziri na Profesa Simon Samwel Msanjila, Katibu Viongozi hawa na Watendaji wote wa Wizara  wananipa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yangu na kutekeleza majukumu yao kwa kujituma, tija na ufanisi. Naahidi Bunge lako kuwa  kwa ari na kasi tuliyonayo tutahakikisha rasilimali za madini zinanufaisha Taifa na mchango wa Sekta ya Madini unaongezeka katika Pato la Taifa, maendeleo ya jamii na kupunguza umaskini nchini.
 
  1. Mheshimiwa Spika,  napenda kutoa pole  kwa Bunge lako Tukufu, familia, ndugu, jamaa na wananchi wa jimbo la Songea Mjini kwa kuondokewa na mpendwa wao,  Mheshimiwa  Leonidas  Tutubert  Gama  (Mb.), na Jimbo la Buyungu, Kigoma kwa kuondokewa na mpendwa wao Mhe. Kasuku Samson Bilago (Mb). Aidha, naomba kuungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kuwapongeza Mheshimiwa Janet Masaburi kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mbunge, Mheshimiwa Dkt. Godwin Ole Mollel, Mbunge wa Jimbo la Siha, Mheshimiwa Stephen Lemomo Kiruswa, Mbunge wa Jimbo la Longido, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mheshimiwa Justin Joseph Monko, Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini na Mheshimiwa Maulid Said Mtulia,  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, kwa kuchaguliwa na kuwa wawakilishi wa wananchi katika Majimbo hayo. Kuchaguliwa na kuteuliwa kwao ni kielelezo cha kuaminiwa na wananchi ili kuwawakilisha ipasavyo katika Bunge hili.
 
  1. Mheshimiwa Spika, napenda kipekee kabisa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mume wangu Mpenzi Balozi Mbelwa Kairuki pamoja na watoto wetu wapendwa kwa kunivumilia, kuniunga mkono na kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili niweze kutekeleza majukumu niliyopewa na Mheshimiwa Rais ya usimamizi wa sekta hii nyeti ya madini.
 
  1. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti  ya  Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18; na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19.
  2.0   DIRA, DHIMA NA MAJUKUMU YA WIZARA   Dira na Dhima ya Wizara  
  1. Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ni kuwa Wizara inayoheshimika Afrika katika kuendeleza rasilimali za madini ili ziweze kuchangia kwa ufanisi katika uchumi wa Taifa na ustawi wa Watanzania. Aidha, Dhima ya Wizara ni kuzibadili rasilimali za madini ziweze kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa na maendeleo endelevu.
  Majukumu ya Wizara  
  1. Mheshimiwa   Spika,   kulingana   na   Hati Idhini (Na.144 ya tarehe 22 Aprili, 2016 iliyofanyiwa marekebisho tarehe 15 Oktoba, 2017, majukumu ya Wizara ya Madini ni: -
  (i)  Kubuni, kuandaa na kusimamia Sera, Mikakati na Mipango ya kuendeleza Sekta ya Madini; (ii) Kusimamia  migodi  na  kuhamasisha  shughuli za  uchimbaji  pamoja  na  utafutaji  wa  madini kwa kutumia tafiti za kijiofizikia na kijiolojia (Geophysical na Geological surveys); (iii) Kuratibu        na     kusimamia        uongezaji       thamani madini kwenye biashara ya madini; kukuza ushiriki wa Wazawa (local content) kwenye shughuli za utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini; (iv) Kusimamia na kuratibu shughuli na maendeleo ya wachimbaji wadogo; kusimamia Taasisi na Mamlaka zilizoko chini ya Wizara; na (v) Kuratibu na kusimamia maendeleo na utekelezaji wa majukumu kwa watumishi wa Wizara.   3.0   MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA WA 2017/18   (a)      Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18  
  1. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18 iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini iliidhinishiwa Bajeti ya jumla ya shilingi 998,337,759,500. Kati ya fedha hizo, shilingi
938,632,006,000 sawa na asilimia 94 ya Bajeti yote ilikuwa ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na shilingi 59,705,753,500, sawa na asilimia 6 ya Bajeti yote ilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.   (b)       Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18  
  1. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ukiondoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za Sekta ya Nishati, Sekta ya Madini ambayo sasa inasimamiwa na Wizara ya Madini, iliidhinishiwa na Bunge lako Tukufu jumla ya shilingi 52,445,367,000. Kati ya fedha  hizo,  shilingi  21,783,000,000  sawa na  asilimia  41.53  ya  Bajeti  yote  zilikuwa  ni  kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo na shilingi
30,662,367,000 sawa na asilimia 58.47 ya Bajeti yote zilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida kwa Wizara na Taasisi zake. Kwa upande wa fedha za Matumizi ya Kawaida, shilingi 13,912,800,000 sawa na asilimia 45.37 zilitengwa kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (O.C) na shilingi 16,749,567,000 sawa na asilimia 54.63 zilitengwa kwa ajili ya Mishahara   (P.E) ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizopo chini yake.  Aidha, Wizara ilipangiwa kukusanya maduhuli ya Serikali ya kiasi cha shilingi 194,663,501,763.  
  1. Mheshimiwa Spika, hadi      kufikia       tarehe
31 Machi, 2018 Wizara   ilipokea jumla ya Shilingi 19,173,608,450.31  kutoka  Hazina  sawa  na asilimia 36.56 ya Bajeti yote ya Wizara ya Shilingi 52,445,367,000 kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18. Kati ya fedha zilizopokelewa, Shilingi 834,976,618 ni fedha za Maendeleo sawa na asilimia 3.83 ya bajeti yote ya Maendeleo ya Shilingi 21,783,000,000. Kwa upande wa Matumizi ya Kawaida, Shilingi 18,338,631,832.31 zilipokelewa sawa na asilimia 59.81 ya fedha zote za Matumizi ya Kawaida zilizotengwa ambazo zilikuwa Shilingi 30,662,367,000. Kati ya fedha  za Matumizi ya  Kawaida  zilizopokelewa  Shilingi  8,227,481,851 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (O.C) na Shilingi 10,111,149,981.31  ni kwa ajili ya Mishahara (P.E) kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake.  
  1. 19. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18, ulizingatia pamoja na mambo mengine: Hati Idhini ya kuanzishwa kwa Wizara ya Madini Namba 144 ya tarehe 22 Aprili,
2016 iliyofanyiwa marekebisho tarehe 15 Oktoba, 2017; Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025; Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 - 2020; Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21); Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; Sera ya Madini ya Mwaka 2009; Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya Mwaka 2017 na Kanuni zake. Vilevile, umezingatia maoni na ushauri wa Kamati Maalum ya Mheshimiwa Rais ya kuchunguza aina, wingi na thamani ya madini   mbalimbali yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Hamis Mruma; Kamati Maalum ya Mheshimiwa Rais ya kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusiana na mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi iliyoongozwa na Profesa Nehemiah Eliakim Osoro; Kamati Maalum ya Spika ya kuchunguza Biashara ya Tanzanite iliyoongozwa na Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko (Mb.) ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Madini; Kamati Maalum ya Spika ya kuchunguza Biashara ya Almasi iliyoongozwa na Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb.); na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.  
  1. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18, maeneo yafuatayo yalipewa kipaumbele: kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Serikali yatokanayo na rasilimali madini; kudhibiti utoroshaji wa madini; kuendeleza wachimbaji wadogo na wa kati wa madini; kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini; kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi wa migodi ikiwemo ukaguzi wa afya, usalama, mazingira na uzalishaji wa madini katika migodi midogo, ya kati na mikubwa; kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika   Sekta   ya   Madini na kuboresha Sera, Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali kuhusu rasilimali madini. Vilevile, kipaumbele kiliwekwa katika kuimarisha Taasisi zilizo chini ya Wizara hususan Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST),  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini (MRI), Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI). Maeneo mengine ya   kipaumbele   yalikuwa   ni   kuwajengea   uwezo
  watumishi wa Wizara katika fani mbalimbali pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya ofisi.   (c)       Ukuaji na Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa  
  1. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2017, Sekta ya Madini ilikua  kwa  asilimia  17.5  ikilinganishwa na asilimia 11.5 ya Mwaka 2016. Kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji wa Sekta ya Madini kulitokana na kuimarishwa kwa udhibiti wa biashara haramu na utoroshwaji wa madini; kuimarishwa kwa ukaguzi na usimamizi katika sehemu za uzalishaji, biashara ya madini; na usafirishaji wa madini nje ya nchi; kuongezeka kwa viwango vya mrabaha na kuanzishwa kwa ada ya ukaguzi wa madini kufuatia marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 yaliyofanyika Mwaka 2017 na Kanuni zake.
 
  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umeendelea kuimarika ambapo katika Mwaka 2017 mchango huo ulifikia asilimia 4.8. Kwa upande wa thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi, mauzo yalifikia Dola za Marekani
1,810,697,000 mwaka 2017. Ni matarajio yetu kuwa thamani ya mauzo itaendelea kuongezeka tena baada ya kukamilisha mageuzi makubwa ambayo tuliyaanzisha ikiwa ni pamoja na uongezaji thamani madini ndani ya nchi.   (d)    Uzalishaji na Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18    
  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwezi
Julai, 2017 hadi Machi, 2018 jumla ya kilo 30,953.59   za dhahabu zilizalishwa na Migodi Mikubwa na ya Kati ya Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, New Luika, North Mara na STAMIGOLD na kusafirishwa nje ya nchi. Vilevile, kilo 2,021.4 za dhahabu zilizalishwa na wachimbaji wadogo wa madini na wachenjuaji wa marudio. Aidha, kiasi cha karati 248,083.94 za almasi kilizalishwa katika Mgodi wa Almasi wa Mwadui (Williamson Diamond Limited) uliopo Shinyanga, pia kiasi cha karati  43,285.31  kilizalishwa  katika  Mgodi  wa  El Hilal na Tanzanite (ghafi) yenye kilogramu 535.99 ilizalishwa na Mgodi wa TanzaniteOne. Vilevile, kiasi cha kilo 516,408.93 cha madini mengineyo ya vito kilizalishwa. Kwa upande wa makaa ya mawe jumla ya tani 385,352 zilizalishwa kwenye Mgodi wa Ngaka Mkoani Ruvuma. Aidha, tani 3,125,399 za madini ya ujenzi na viwandani zilizalishwa. Uzalishaji huu kwa ujumla wake uliiwezesha Serikali kukusanya mrabaha wa Shilingi 175,518,751,221.49.  
  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na mageuzi ambayo tumeyafanya, Wizara iliratibu mnada wa madini ya vito ya tanzanite uliofanyika tarehe 18 hadi
21 Desemba, 2017. Lengo la mnada huo lilikuwa ni kukuza biashara ya ushindani baina ya wachimbaji na wauzaji wa madini haya na wanunuzi wa kimataifa ili kupata bei bora zaidi na ya ushindani kwa njia ya uwazi na kuwapatia wachimbaji wa madini ya tanzanite soko la uhakika. Katika mnada huo, tanzanite yenye uzito wa kilo 47 iliuzwa kwa jumla ya Dola za Marekani 820,744 sawa na shilingi 1,839,476,075. Mapato yaliyokusanywa na Serikali ni mrabaha wa shilingi  110,368,564.50,  ada  ya  ukaguzi  shilingi 18,394,760.75 na ushuru wa   huduma wa shilingi 5,518,428.20.  
  1. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa maduhuli ya Sekta  ya  Madini,  katika  Mwaka  wa  Fedha  wa
2017/18 Wizara ya Madini, ilipangiwa kukusanya jumla ya shilingi 194,663,501,763 na Bunge lako Tukufu kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vikiwemo mrabaha; ada ya mwaka; ada za kijiolojia; ada ya uchambuzi wa madini; uchapishaji na uuzaji wa nyaraka za zabuni; stakabadhi nyinginezo; marejesho ya fedha za Serikali; tozo mbalimbali zinazotokana na adhabu na ada za ukaguzi. Napenda kulitaarifu Bunge lako tukufu kuwa hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2018 jumla ya maduhuli ya shilingi 225,006,324,173.21 yalikuwa yamekusanywa. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 115.59 ya lengo lililowekwa katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.  
  1. Mheshimiwa Spika, ongezeko la makusanyo ya maduhuli limetokana na kuongezeka kwa viwango vya mrabaha kutoka asilimia nne hadi sita kwa madini ya metali, na kutoka asilimia tano hadi sita kwa madini ya vito; kuanzishwa kwa tozo ya ukaguzi ya asilimia moja ya mauzo ya madini; usimamizi wa biashara ya madini na kuimarisha udhibiti wa utoroshwaji wa madini kwa kushirikiana na wananchi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
  (e)    Udhibiti wa Biashara ya Madini    
  1. Mheshimiwa  Spika, Wizara  imeendelea kufanya ukaguzi wa uzalishaji wa madini kwenye migodi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata  takwimu  sahihi  za  madini  yanayozalishwa na kuuzwa  ndani na nje ya nchi; thamani halisi ya madini hayo; na mrabaha stahiki unaopaswa kulipwa. Ukaguzi huo hususan kwenye migodi na mitambo ya
  uchenjuaji  umekuwa  ukifanyika  kwa  kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Kufuatia jitihada hizo, makusanyo ya mrabaha yameongezeka. Kwa mfano, hadi kufikia mwezi Machi, 2018 Ofisi ya Madini (Chunya)  imeweza  kukusanya  kiasi  cha  shilingi 718,667,100.41 na Ofisi ya Madini (Mwanza) kiasi cha shilingi 9,843,380,762.80 ikilinganishwa na shilingi 416,968,335.28 na shilingi 6,181,589,371.75 zilizokusanywa na Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17, sawia. Wizara pia imeanzisha utaratibu mpya wa uombaji wa vibali vya kusafirisha madini nje ya nchi, ambapo mchimbaji au mfanyabiashara wa madini hulazimika kuwasilisha sampuli GST kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kufahamu ubora stahiki wa sampuli au madini yanayoombewa kibali cha kusafirishwa nje ya nchi. Vilevile, katika kudhibiti shughuli za uzalishaji na biashara ya madini ya tanzanite ambayo hupatikana Tanzania pekee, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ilijenga ukuta wenye mzingo wa kilomita 24.5 katika Migodi ya Mirerani kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini ya tanzanite kwenda nje ya nchi.  
  1. Mheshimiwa Spika, Serikali  kupitia  Wizara ya Madini ilizuia uingizaji wa madini yanayopatikana nchini kama vile makaa ya mawe na jasi ili kuhakikisha madini haya yananunuliwa hapa nchini kwa lengo la kukuza soko la ndani la madini hayo. Kutokana na udhibiti huo, jumla ya tani 431,029.14 za makaa ya  mawe  zenye  thamani  ya  Dola  za  Marekani
18,314,709.53 ziliuzwa hadi kufikia Machi, 2018 ikilinganishwa na tani 429,682.85 zilizouzwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 zenye thamani ya Dola za Marekani 16,931,162.29. Vilevile, tani 121,186.82 za   jasi zenye thamani ya Dola za Marekani 3,120,024.09 ziliuzwa kufikia Machi, 2018 ikilinganishwa na tani 181,080.34 zilizouzwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 zenye thamani ya Dola za Marekani 5,283,526.13. Wizara imeanza maandalizi ya uanzishwaji wa masoko ya madini ya dhahabu na vito ikiwemo tanzanite, almasi na madini mengine. Maandalizi haya yanashirikisha Timu ya Wataalamu na wadau mbalimbali wa biashara ya madini na Serikali.  
  1. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha udhibiti dhidi ya utoroshwaji wa madini, Serikali imeendelea na mkakati wa kukabiliana na biashara haramu ya madini ambapo Wizara kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inaendelea kufanya ukaguzi kupitia madawati yaliyopo katika viwanja vya ndege, Bandari na mipaka ya nchi. Kufuatia kaguzi hizo, jumla ya matukio 9 ya biashara haramu ya madini yenye thamani ya Dola za Marekani 229,037.85 na shilingi
1,500,000,000 yaliripotiwa kutokea katika Vituo vya Kutokea (Exit Points) nchini katika kipindi cha Julai, 2017  hadi  Aprili,  2018  ikilinganishwa  na  matukio 11 ya biashara haramu ya madini yenye thamani ya shilingi 268,700,000 yaliyotokea Mwaka wa Fedha wa 2016/17. Aidha, Serikali imekuwa ikiwafikisha wahusika wa matukio hayo katika Vyombo vya Sheria. Wizara bado inaona kuna changamoto ya utoroshwaji wa madini pamoja na kupungua kwa matukio ya ukamataji kwa watoroshaji madini. Hivyo, azma ya Wizara ni kuimarisha udhibiti kwenye mipaka yote ili hatimaye kuondoa kabisa mianya ya utoroshwaji wa madini nchini.  
  1. Mheshimiwa Spika, pamoja  na  uimarishaji huo, bado kuna changamoto mbalimbali katika udhibiti wa shughuli za madini nchini. Hivyo, natoa rai na kuwaomba wadau wote wa Sekta ya Madini na wananchi wote kushiriki katika ulinzi wa rasilimali madini ili ziweze kuwa na manufaa makubwa zaidi kwa Taifa.
  (f )       Ujenzi wa Ukuta kwenye Migodi ya Mirerani    
  1. Mheshimiwa Spika,   itakumbukwa   kuwa mwezi Juni, 2017 uliunda Kamati Maalum ya Bunge iliyoshughulikia namna shughuli za uchimbaji na uuzaji wa madini ya tanzanite zinavyofanyika nchini. Kamati hiyo ilitoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa mfumo mpya wa udhibiti wa madini ya tanzanite.
 
  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na mapendekezo hayo, tarehe 20 Septemba, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli aliliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kujenga ukuta kuzunguka eneo la migodi ya tanzanite Mirerani ili kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo. Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Ukuta huo ulianza kujengwa kuanzia tarehe 1 Novemba, 2017 na kukamilika tarehe 15 Februari, 2018 na kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais tarehe 6 Aprili, 2018.
 
  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na udhibiti huo, katika kipindi kifupi cha miezi mitatu tu cha Januari hadi Machi 2018, Wizara imefanikiwa kukusanya mrabaha wa kiasi cha jumla ya shilingi 714,670,000. Katika kiasi hicho, shilingi 614,670,000 zinatokana na makusanyo kutoka kwa wachimbaji wadogo. Kiasi
  hicho kilichokusanywa kinazidi jumla ya makusanyo ya   mrabaha   wa   miaka   mitatu   iliyopita   kutoka kwa wachimbaji wadogo. Pia, Bunge lako Tukufu litapendezwa kufahamu kwamba katika Mwaka 2015 tulikusanya mrabaha wa shilingi 166,850,000; Mwaka 2016 shilingi 71,860,000; na Mwaka 2017 shilingi 147,140,000 kutoka kwa wachimbaji wadogo.   (g)    Kuimarisha Usalama Migodini    
  1. Mheshimiwa Spika, pamoja na majukumu mengine Wizara hii ina wajibu wa kuhakikisha usalama wa shughuli za uchimbaji migodini. Kwa msingi huo, Wizara imeendelea kufanya kaguzi mbalimbali ambapo kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 jumla ya leseni za migodi 2,204 zilikaguliwa. Kati ya leseni hizo, 6 ni za uchimbaji mkubwa, 134 za uchimbaji wa kati na 2,064 za uchimbaji mdogo. Wizara pia iliendelea kufanya uchunguzi wa ajali na matukio yanayotokea migodini kwa lengo la kubaini changamoto za kiusalama ili kuweza kuzuia matukio ya aina hiyo katika migodi. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, jumla ya ajali 14 ziliripotiwa na kuchunguzwa katika migodi. Uchunguzi huo uliofanyika ulibaini kuwa wachimbaji 33 walifariki dunia; 50 walijeruhiwa, kutibiwa na kuendelea na kazi zao. Matukio hayo ni kama ifuatavyo: Kanda ya Kati (Singida na Dodoma) matukio 5; Kanda ya Kaskazini (Arusha, Manyara na Kilimanjaro) matukio 3; Kanda ya Kusini Magharibi (Mbeya, Songwe na Iringa) matukio
2; Kanda ya Kati Magharibi (Shinyanga na Tabora) tukio 1; na Kanda ya Ziwa Victoria Mashariki (Mara na Simiyu) tukio 1. Uchunguzi wa ajali hizo, ulibaini kuwa chanzo kikubwa cha ajali hizo ni kutozingatia kanuni za usalama. Kufuatia uchunguzi huo, ripoti ziliandaliwa   na wahusika walipewa nakala ya ripoti husika ili kuboresha usalama katika maeneo yao na wengine 42  leseni  zao  zilisimamishwa  hadi  waliporekebisha na  kufuata  kanuni  za  usalama  migodini  ambapo jumla ya leseni 38 zilikidhi matakwa ya kiusalama na kuruhusiwa kuendelea na kazi. Mathalan, katika eneo la Irasanilo - Solemba, Buhemba shughuli za uchimbaji zilisimamishwa kwa muda wa mwaka mmoja ili kurekebisha kasoro za kiusalama.  
  1. Mheshimiwa Spika, kanuni ya 71 ya Kanuni za Afya, Usalama na Utunzaji wa Mazingira za Mwaka
2010 inaelekeza wachimbaji kutoa taarifa ya kusudio la kubadilisha teknolojia yoyote katika shughuli za uchimbaji na uchenjuaji na kuwasilisha taarifa hiyo kwenye Ofisi za Madini. Hata hivyo, kumekuwa na hulka ya wachimbaji kutumia teknolojia ya vifaa mbalimbali katika shughuli za uchimbaji bila kuzingatia uwezo na ubora wa vifaa hivyo. Hali hii inasababisha uwepo wa ajali nyingi ambazo zingeweza kuepukika. Mathalan, ajali iliyotokea tarehe 06 Aprili, 2018 Wilayani Bahi, ilisababishwa na winchi inayotumika kubebea mizigo kutumika kubebea watu. Katika uchunguzi ilibainika kuwa wahusika walikuwa hawafanyi ukaguzi wa kamba mara kwa mara. Timu yangu ya ukaguzi ilipowahoji wahusika walionusurika kwenye ajali hiyo, ilibaini kuwa wahusika hao hawakuwa na taarifa kuhusu uwezo wa winchi husika kunyanyua mizigo ila yalikuwa ni mazoea ya kutumia chombo hicho. Natoa rai kwa wachimbaji na wawekezaji wote katika Sekta ya Madini nchini kufuata maelekezo ya Kanuni za Afya, Usalama na Utunzaji wa Mazingira zilizopo ili wawe salama katika shughuli zao za uchimbaji.   (h)      Kuimarisha Masuala ya Afya Migodini  
  1. Mheshimiwa Spika, ili kupunguza athari za kiafya zinazoweza kuwapata wafanyakazi migodini kutokana na uvutaji wa vumbi na hewa chafu kuzidi kiwango stahiki kwa muda mrefu; ukaaji wa muda mrefu kwenye eneo lenye kelele nyingi; na kutumia vifaa vyenye viwango vya chini kulingana na mahitaji ya eneo husika, Wizara yangu imeimarisha ukaguzi wa mazingira ya kazi migodini pamoja na kuhamasisha uwepo na matumizi ya vifaa kinga. Ikumbukwe pia, utumiaji wa vifaa vya kinga ni sehemu ya kuzuia athari za kiafya. Kutotumia vifaa vya kinga kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya kama kuathiri mfumo wa kupumua au kuambukizana magonjwa kama Kifua Kikuu (TB) ikizingatiwa kuwa wanafanya kazi kwenye maeneo yenye changamoto ya ujazo wa hewa. Ukaguzi wa mara kwa mara kuhusiana na utumiaji wa vifaa vya kinga umekuwa ukifanyika migodini. Aidha, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na utafiti ili kubaini ukubwa wa changamoto ya TB migodini na kutoa ushauri wa namna bora ya kujikinga na maradhi hayo.
 
  1. Mheshimiwa Spika,   kwa   kushirikiana   na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto tunaendelea kuimarisha ukaguzi wakati wa kuajiriwa; na upimaji wa afya mara kwa mara kwa wafanyakazi wote wa migodini. Pia, Wizara inaendelea kuweka utaratibu wa kuchunguza afya wakati mfanyakazi anaacha au kuachishwa kazi. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji madini zinafanywa kwa kujali afya za wafanyakazi.
  (i)       Kuimarisha Utunzaji wa Mazingira Migodini na Kwenye Miradi ya Uchenjuaji Madini  
  1. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Madini ya Mwaka
2010 pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2017 na  Kanuni  zake  zinasisitiza  umuhimu  wa  utunzaji wa mazingira. Kama nilivyoeleza awali, shughuli za utafiti, uchimbaji na uchenjuaji wa madini zinapaswa kuhakikisha usalama wa watu na mazingira katika maeneo wanayofanyia kazi. Kwa mujibu wa Kifungu cha 60 cha Sheria ya Madini, moja ya masharti ya leseni zitolewazo kwa wachimbaji madini ni kutoa tamko la utunzaji wa mazingira ambapo kwa mchimbaji mdogo hutakiwa kuwasilisha Mpango wa Utunzaji wa Mazingira (Environmental Protection Plan) kwa Afisa Madini  Mkazi.  Kwa  upande  wa  uchimbaji  wa  kati na  mkubwa,  wamiliki  hutakiwa  kuandaa  Tathmini ya Athari za Mazingira na Mpango wa Kutunza Mazingira (Environmental Impact Assessment (EIA) and Environmental Management Plan (EMP)). Lengo kuu la kuwa na maandiko haya ni kuhakikisha mwenye mradi anatambua  kuwa  shughuli  anazofanya  zina  athari kwa mazingira na kufahamu maandalizi yake kwenye utunzaji na uhuishaji wa mazingira ili kuwa rafiki kwa matumizi ya binadamu akiwa bado anaendelea kuwekeza au anapomaliza uchimbaji katika eneo husika.  
  1. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Kanuni ya 177
– 184 za Mwaka 2010 za Uchimbaji Salama, Afya na Utunzaji wa Mazingira zinazoelekeza migodi kuwa na miundombinu muhimu ya kutupa mabaki ya miamba, mabwawa ya kutunzia maji na mabaki yenye kemikali yatokanayo na uchenjuaji wa madini (Waste Rocks   Dumps and Tailings Storage Facilities). Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Wizara yangu ilimuelekeza mmiliki wa Mgodi wa Dhahabu wa Nyarugusu kulipa fidia kwa waathirika kutokana na bwawa la kuhifadhia maji yenye kemikali zilizotumika kuchenjua madini ya dhahabu kumwaga maji hayo katika mashamba na kuathiri mazao ya wakulima kutokana na mvua kubwa kunyesha ndani ya muda mfupi. Licha ya kulipa fidia kwa waathirika, mmiliki alielekezwa kufanya usanifu mpya wa bwawa hilo ili liweze kuhimili mvua kubwa pamoja na kuandaa mpango wa dharura wa ukusanyaji maji hayo wakati wa mvua. Pia, Wizara imeendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye maeneo hayo ili kuona uhimilivu wa miundombinu husika.  
  1. Mheshimiwa Spika, hali kadhalika, Wizara yangu imeendelea kuhakikisha kuwa migodi ya madini inapofungwa, mazingira ya eneo husika yanaachwa katika hali ya usalama. Kwa mujibu wa Kanuni ya 206 ya Kanuni za Madini (Usalama wa Afya Mgodini na Utunzaji wa Mazingira) za Mwaka 2010, Migodi ya kati na mikubwa inatakiwa kuwasilisha Mpango wa Ufungaji Migodi (Mine Closure Plan). Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Kampuni ya ACACIA inayomiliki Migodi ya dhahabu ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ilishawasilisha Mpango wake wa Ufungaji Mgodi na kuweka Hati Fungani ya Mazingira. Pia, Mgodi wa Dhahabu  wa  Geita  Gold  Mining  Limited (GGM)  uko kwenye hatua za kukamilisha utaratibu wa kuweka Hati Fungani. Vilevile, Migodi ya Dangote, TanzaniteOne, New Luika na Williamson Diamonds nayo inakamilisha majadiliano ili kuhakikisha usalama na utunzaji wa mazingira unazingatiwa.
  (j)        Usimamizi wa Matumizi ya Baruti    
  1. Mheshimiwa Spika, udhibiti  wa  matumizi ya baruti kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo za utafutaji wa mafuta na gesi na uchimbaji wa madini ili kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa usalama na kwa madhumuni yaliyokusudiwa uliendelea kufanyika. Katika ukaguzi uliofanywa na Wizara, ilibainika kuwa jumla ya tani 22,474 za baruti na vipande 1,749,203 vya fataki vilitumika kwenye shughuli mbalimbali. Aidha, jumla ya maghala 37 ya kuhifadhia baruti na fataki yalikaguliwa katika Mikoa yote yenye shughuli za uchimbaji wa madini ili kubaini utunzaji salama kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Baruti ya Mwaka
1963 na Kanuni zake.   (k)      Uendelezaji wa Wachimbaji Wadogo  
  1. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kuwa Sekta ya Madini inatoa ajira kati ya 500,000 na 1,500,000 kutokana na utafiti uliofanywa na UNEP Mwaka 2012, Wizara itaendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo kujiajiri kupitia Sekta ya Madini kwa kuwatambua, kuwaendeleza, kuwarasimisha na kuwapatia maeneo ya uchimbaji wa madini. Vilevile, Wizara itaendelea kuwapatia taarifa za kijiolojia, kiufundi na kuwawezesha kupata huduma za kifedha na masoko. Aidha, Wizara itaendelea kuwapatia mafunzo   ya   teknolojia   na maarifa ya kisasa kwa ajili ya kuendeleza shughuli za uchimbaji ili wakue na waweze kuwa wachimbaji wa kati na wakubwa katika siku za usoni. Serikali inaamini kuwa uchimbaji mdogo siyo hadhi ya kudumu bali ni hatua ya mpito kuelekea katika uchimbaji wa kati hadi mkubwa. Sababu za kufanya hivyo zipo wazi kwa kuwa wachimbaji wadogo endapo watafanikiwa kukua,
  mapato yao yanaweza kuwekezwa zaidi  kwenye Sekta ya Madini na sekta nyingine nchini na hivyo kuchangia zaidi kwenye ukuaji wa Sekta ya Madini, ukuaji wa uchumi na Pato la Taifa na hatimaye kuwanufaisha watanzania wengine.  
  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia GST na STAMICO chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ilikamilisha utafiti wa kina wa kijiosayansi uliohusisha uchorongaji na ukadiriaji wa mbale katika maeneo ya wachimbaji wadogo kwenye maeneo sita ya ujenzi wa Vituo vya Umahiri vya Katente (Bukombe), Itumbi (Chunya), Kona Z (Tanga), Kapanda (Mpanda), Buhemba (Musoma) na Kyerwa (Bukoba). Vituo hivyo vitatumika kwa ajili ya mafunzo ya uongezaji thamani madini na uchimbaji salama pamoja na kuongeza uzalishaji, tija na hivyo kuongeza mapato kwa wachimbaji wadogo. Ukadiriaji wa mbale umeonesha kuwepo kwa  takriban wakia
47,605 za dhahabu katika maeneo ya Mpanda (D – Reef na Kapanda); wakia 10,737.33 za dhahabu katika eneo la Buhemba; wakia 46,663 za dhahabu eneo la Chunya (Itumbi); na wakia 9,459 za dhahabu katika eneo la Katente. Aidha, ukadiriaji wa mbale katika maeneo  ya  Tanga  (Kiomoni,  Kange  na  Mkulumuzi) na Kyerwa (Kaborishoke) umeonesha uwepo wa tani 403,056,469  za  miamba  chokaa  yenye  ubora  wa zaidi ya asilimia 48 ya chokaa (calsium); na tani 1,409,742.15 za bati sawia. Maandalizi ya ujenzi wa Vituo hivyo yanaendelea.   Aidha, matokeo ya utafiti huo yatatumika kuainisha njia bora za uchenjuaji kwenye kila eneo na kuwasaidia wachimbaji wadogo kupunguza upotevu wa madini wakati wa uchenjuaji.  
  1. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa unaendelea  kujengwa  ambapo  kwa
  sasa umefikia asilimia 70. Gharama za mgodi huo ni Dola za Marekani 584,800. Mgodi huu utawezesha Chama cha Washirika wa Kijiji cha Lwamgasa na wachimbaji wanaozunguka Mgodi huo kuchimba na kuchenjua dhahabu kwa kutumia teknolojia sahihi na yenye gharama nafuu. Vilevile, mafunzo mbalimbali yamekuwa  yakitolewa  kwa  wachimbaji  wadogo ambapo kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18. Jumla ya wachimbaji wadogo 4,468 walipatiwa mafunzo katika Mikoa 13 ambayo ni Manyara, Morogoro, Tanga, Pwani, Shinyanga, Geita, Mara, Katavi, Singida, Dar es Salaam, Mbeya, Lindi na Mtwara. Vilevile, STAMICO kwa kushirikiana na Tanzania Gender Network Program  (TGNP)  na  Women  in  Mining  Association (WIMA) ilitoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Mwalazi mkoani Morogoro ambapo jumla ya wachimbaji 37 walipatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuchakata madini ya dolomite kwa kuzingatia matumizi na mahitaji ya soko.  
  1. Mheshimiwa Spika, mafunzo mengine yalito- lewa na Ofisi ya Madini Mirerani kwa kushirikiana na Wakala wa Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) katika eneo la Mirerani; Ofisi ya Madini Geita kwa kushirikiana na OSHA katika Mkoa wa Geita; Ofisi ya Madini Shinyanga kwa kushirikiana na OSHA na TRA katika Mkoa wa Shinyanga; Ofisi ya Madini Chunya kwa kushirikiana na Kampuni ya PAULSAM katika Wilaya ya Chunya; Ofisi ya Madini Singida kwa kushirikiana na Vyama vya Wachimbaji Wadogo na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) katika Mkoa wa Singida; Ofisi ya Madini Mpanda katika Wilaya ya Mpanda; Ofisi ya Madini Songea; Ofisi ya Madini Musoma katika Wilaya za Butiama, Tarime na Bunda; Ofisi ya  Madini  Mtwara  katika  Mikoa  ya  Lindi  na
  Mtwara; na Ofisi ya Madini Dar es Salaam katika Mikoa ya Morogoro, Tanga na Pwani. Mafunzo hayo yalihusu usalama na afya mahali pa kazi.   (l)     Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali kuhusu Rasilimali Madini    
  1. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Serikali chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa Rais, imefanya mageuzi makubwa na ya msingi kwenye Sekta ya Madini. Tunalishukuru Bunge lako Tukufu kwa kuridhia na kupitisha Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kupitia Marekebisho ya Sheria mbalimbali yaliyofanywa na Sheria ya Marekebisho Na.7 ya Mwaka 2017. Katika kuwezesha utekelezaji wa Sheria hiyo, Wizara ya Madini ilitengeneza Kanuni za Madini zipatazo saba ambazo ni:-
  (i)  Kanuni za Madini (Haki Madini) za Mwaka 2018;   (ii)  Kanuni       za    Madini      (Biashara      ya    Madini      na Makinikia) za Mwaka  2018;   (iii)  Kanuni za Madini (Huduma na Bidhaa Madini zinazotolewa na Watanzania) za Mwaka 2018;   (iv)  Kanuni  za  Madini  (Madini  Mionzi)  za  Mwaka 2018;   (v)  Kanuni za Madini (Uongezaji Thamani Madini) za Mwaka 2018;   (vi)  Kanuni za Madini (Utafiti wa Kijiolojia) za Mwaka 2018; na   (vii)  Kanuni za Madini (Ukaguzi na Uchunguzi wa Nyaraka) za Mwaka 2018.  
  1. Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 105 (1) na (2) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya Mwaka 2017 kinamtaka mmiliki wa leseni ya utafutaji na uchimbaji wa madini kuandaa Mpango wa Mwaka wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR). Mpango huo lazima ukubalike kwa pamoja na Mamlaka ya Serikali ya Mtaa husika au Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushauriana na Waziri anayehusika na Serikali za Mitaa na Waziri anayehusika na masuala ya fedha. Aidha, Kifungu cha 105(4) kinaitaka kila Halmashauri ya Serikali ya Mtaa kuandaa Mwongozo wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii, kusimamia utekelezaji wa Mpango Kazi wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii na kutoa elimu kwa umma kuhusu miradi iliyopo katika maeneo yao. Hivyo, Wizara ya Madini inawahimiza wadau wote wa Sekta ya Madini wazingatie Sheria ya Madini wanapotekeleza majukumu yao.
  (m)  Uimarishaji wa Usimamizi wa Sekta ya Madini  
  1. Mheshimiwa Spika, Marekebisho  ya  Sheria ya Madini ya Mwaka  2017 yamewezesha kufanyika kwa mabadiliko katika usimamizi wa Sekta ya Madini ambapo majukumu ya iliyokuwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na baadhi ya majukumu ya Kamishna wa Madini yamehamishiwa Tume ya Madini. Pia, Ofisi zilizokuwa za Kanda na Ofisi za Maafisa Madini Wakazi zipo chini ya Tume ya Madini. Kutokana na mabadiliko hayo, kila Mkoa utakuwa na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi na kila mgodi mkubwa na wa kati utakuwa na Afisa Mgodi Mkazi. Mabadiliko hayo yamelenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hususan kuimarisha ukusanyaji wa  maduhuli  ya  Serikali;  kuondoa  muingiliano  wa
  majukumu na kuimarisha usimamizi wa rasilimali madini ili kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.   (n)   Uongezaji Thamani Madini  
  1. Mheshimiwa Spika, Serikali  imeendelea  na jitihada mbalimbali za kuhakikisha shughuli za uongezaji   thamani   madini   zinafanyika   ndani   ya nchi  ikiwa  ni  pamoja  na  kusimamia  ipasavyo  zuio la kusafirisha madini ghafi nje ya nchi. Wizara ilitoa matangazo ya kukaribisha uwekezaji katika ujenzi wa vinu vya uchenjuaji kwa ajili ya kusafisha na kuongeza thamani madini ya metali - smelter na refineries hapa nchini. Jumla ya maombi 27 ya uwekezaji kwenye smelter na refineries yaliwasilishwa na uchambuzi unaendelea kufanyika ili kupata mwekezaji atakayekidhi vigezo.
 
  1. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa madini ya vito, Wizara imeendelea kukijengea uwezo Kituo cha   Jimolojia   Tanzania   (TGC)   kilichopo   Arusha kwa kuimarisha miundombinu yake. Vilevile, Kituo kimepata usajili wa kudumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa namba ya usajili REG/SAT/033 wa kutoa mafunzo ya Diploma in Gem
& Jewellery Technology mwezi Oktoba, 2017. Mafunzo hayo yatakuwa ya muda wa miaka 3 na yanatarajiwa kuanza   mwezi   Agosti,   2018.   Katika   kuwajengea uwezo wakufunzi wazawa, Wizara iliingia Mkataba na Kampuni ya Centre for Development of Gem & Jewellery Technology kutoka nchini India kuleta wakufunzi saba (7) ambao watatoa mafunzo mbalimbali ya vito na usonara katika Kituo hiki wakishirikiana na wakufunzi wazawa. Aidha, Kituo kimeendelea kutoa mafunzo ya usanifu wa madini ya vito (lapidary) katika ngazi ya Astashahada ambapo jumla ya wanafunzi wanawake   18 walidahiliwa chini ya ufadhili wa Wizara ya Madini pamoja na Kamati ya maonesho ya Madini ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair).   (o)    Kazi zilizotekelezwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini - SMMRP  
  1. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18 kazi zilizotekelezwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ni pamoja na upatikanaji wa Washauri Waelekezi kwa ajili ya kusanifu na kusimamia ukarabati na upanuzi wa Ofisi 7 za Madini za Mikoa kuwa Vituo vya Umahiri ambazo ni Bariadi, Bukoba (Tazama Picha Na.1), Chunya, Mpanda, Musoma, Tanga na Songea. Pia, Mradi uligharimia upatikanaji wa Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya Chuo cha Madini Kampasi ya  Dodoma.  Michoro  ya  majengo hayo imekamilika na makadirio ya gharama za ujenzi yanaendelea kufanyika. Kazi nyingine iliyofanyika ni kusimamia ujenzi wa Mgodi wa Umahiri katika eneo la Lwamgasa - Geita ambao utagharimu Dola za Marekani 584,800 kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo ambapo ujenzi wa shimo la uchimbaji (mining shaft) umefikia asilimia 70 (Tazama Picha Na.2); kuiwezesha GST kufanya utafiti wa kijiolojia kwa ajili ya ukadiriaji wa mbale katika maeneo yanayokusudiwa kuanzishwa Vituo vya Mfano. Maeneo hayo ni Bukombe (Katente); Chunya (Itumbi); Mpanda (D-Reef na Kapanda); Musoma (Buhemba); Kyerwa (Kyerwa); na Tanga (Kiomoni, Kange na Mkulumuzi). Taarifa ya utekelezaji wa utafiti huo imebainishwa kwa kina katika sehemu ya taarifa ya utekelezaji wa kazi zilizofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafutaji Madini Tanzania.
    Picha Na.1: Picha ya Muonekano wa Ofisi ya Madini itakayojengwa Bukoba.
  Picha Na.2: Picha ya Muonekano wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Mgodi wa Mfano, Lwamgasa – Geita.  
  1. Mheshimiwa Spika, ili kuboresha mazingira ya kazi na kuimarisha utendaji kazi katika Sekta ya Madini, Mradi ulinunua vifaa mbalimbali vya ofisi ambavyo ni vifaa vya ukaguzi, maabara na kemikali kwa ajili ya Wizara, Taasisi za GST, MRI, TGC na Ofisi za Madini za Mikoa. Vifaa hivyo ni vya kupimia viwango vya madini kwenye sampuli mbalimbali na vya ukaguzi wa migodi. Thamani ya vifaa hivyo ni Dola za Marekani 350,000. Vilevile, Mradi uliwezesha kuandaa Mwongozo wa namna bora ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo nchini (Training Manual Handbook). Mwongozo huo utawasaidia wachimbaji wadogo namna ya kufanya utafiti wa awali; uchimbaji na uchenjuaji endelevu; kuzingatia afya na usalama migodini; utunzaji bora wa mazingira; utunzaji wa kumbukumbu za fedha na ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali. Mwongozo huo utakamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2018.
  (p)       Ajira na Maendeleo ya Watumishi  
  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2017/2018, Wizara imepata Kibali cha Ajira Mpya chenye jumla ya nafasi 16 katika kada za Katibu Mahsusi 3, Jiokemia 1, Mjiolojia 1, Wahandisi Migodi 2, Watunza Kumbukumbu Wasaidizi 2, Madereva 6 na Mkutubi Msaidizi 1. Vilevile, katika Ikama  ya  Watumishi  kwa  Mwaka  wa  Fedha  wa
2017/18, Wizara imeidhinishiwa nafasi za ajira mpya 53, kuwapandisha vyeo watumishi 196, kubadilisha kada watumishi 7 na nafasi za uteuzi 3. Aidha, katika Ikama ya Watumishi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18, STAMICO iliidhinishiwa nafasi 36 za kuwapandisha vyeo watumishi. Pia, GST imeidhinishiwa nafasi 36 za kuwapandisha vyeo watumishi, kuwabadilisha kada watumishi 3 na nafasi 6 za uteuzi.  
  1. Mheshimiwa Spika,   Wizara    imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake 44 katika fani mbalimbali ikiwemo Jiolojia na Utafutaji wa Madini; upimaji wa ardhi (jomatikia); Sayansi ya Mazingira; Uhasibu; Utawala; Sera za Uchumi; Takwimu na Uhazili. Kati ya hao, watumishi 40 wamehudhuria mafunzo ya muda mrefu katika ngazi za Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili. Watumishi 4 walipata mafunzo ya muda mfupi kuhusu utafiti wa kijiolojia na usimamizi wa rasilimali madini yaliyofanyika nchini China.
 
  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa huduma ya lishe, chakula na malipo ya dawa zilizo nje ya orodha ya dawa zinazogharamiwa na Bima ya Afya kwa watumishi wanaoishi na virusi vya UKIMWI na UKIMWI, ikiwa ni utekelezaji wa Waraka wa Watumishi wa Umma Namba 2 wa Mwaka 2006 na Mwongozo wa Kudhibiti UKIMWI Katika Utumishi wa Umma wa Mwaka 2007.
    KAZI ZILIZOTEKELEZWA NA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA    
  1. Mheshimiwa Spika,   Wizara   ya   Madini inasimamia jumla ya Taasisi 6. Taasisi hizo ni Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Madini Tanzania, Shirika la Madini la Taifa, Chuo cha Madini, Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia na Kituo cha Jimolojia Tanzania.
  (a) Tume ya Madini  
  1. Mheshimiwa Spika, Tume ya Madini imeundwa kwa mujibu wa  Kifungu  cha  21  cha  Sheria  ya
  (Marekebisho ya Sheria mbalimbali) ya Mwaka 2017 iliyorekebisha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, na ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 30 Aprili,
  1. Kazi zilizotekelezwa na Tume ni pamoja na kupitia, kuchambua na kuhakiki maombi ya leseni za utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini yaliyowasilishwa na waombaji wa leseni baada ya tarehe 4 Julai, 2017. Uhakiki uliofanywa na Tume umebaini kuwepo kwa jumla ya maombi 4,394 ya Leseni za Uchimbaji Mdogo (PML) yaliyokuwa yamependekezwa  kupewa  leseni. Pia, kulikuwa na maombi 549 ya leseni za biashara ya madini yaliyokidhi vigezo vya kupewa leseni hizo. Maombi hayo yote yanaendelea kuandaliwa leseni husika.
 
  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, Tume ilichambua na ilihakiki maombi ya leseni za utafutaji na uchimbaji wa kati wa madini yaliyowasilishwa baada ya tarehe
4 Julai, 2017. Uhakiki huo ulibaini uwepo wa jumla ya maombi 150 ya leseni za utafutaji wa madini na 15 za uchimbaji wa kati za madini. Aidha, uchambuzi wa maombi ya leseni ulibaini kuwepo kwa migogoro 4 katika maeneo yaliyoombewa leseni; taarifa za upembuzi yakinifu zisizojitosheleza; kutokuwepo kwa taarifa za Mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii katika kutoa huduma (Corporate Social Responsibility – CSR); kutokuwepo kwa Mpango wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika miradi ya madini (Local Content Plan); na kutokuwepo kwa tamko la kiapo cha uadilifu – “Integrity Pledge”. Waombaji wa leseni wamejulishwa kupitia Vyombo vya Habari kuhusu mapungufu hayo ili wawasilishe taarifa hizo zinazohitajika kwa mujibu wa Sheria.   (b)        Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Madini Tanzania – (GST)  
  1. Mheshimiwa Spika, majukumu  ya msingi  ya
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ni:-   (i)      kukusanya,  kuchambua,  kutafsiri  na  kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za jiosayansi (jiolojia, jiokemia na jiofizikia) na za upatikanaji madini;   (ii)      kutengeneza na kusambaza ramani mbalimbali za jiosayansi; kufanya uchunguzi wa maabara kwa sampuli mbalimbali za miamba, madini, maji, mimea na udongo kwa ajili ya tafiti mbalimbali;   (iii)      kutoa  idhini  ya  maandishi  kwa  sampuli  za miamba, udongo na sampuli zilizo katika hali ya vimiminika kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi;   (iv)     kusaidia wachimbaji wadogo hasa katika kubaini umbile na aina ya mbale, kutambua aina na ubora wa madini pamoja na namna bora ya uchenjuaji;   (v)      kuratibu  majanga  asilia  ya  jiolojia  (kama  vile matetemeko                      ya  ardhi,   milipuko   ya  volkano, maporomoko ya ardhi) na kutoa ushauri wa namna bora ya kujikinga;   (vi)      kuboresha kanzidata ya Taifa ya jiosayansi na madini;   (vii)      kufanya tafiti maalum za jiosayansi;   (viii)      kufanya tafiti za jioteknolojia na kutoa ushauri unaostahili                          katika   masuala   ya   ujenzi   wa miundombinu na makazi; na   (ix)       kutoa ushauri wa jiosayansi na utafutaji madini kwa wadau.  
  1. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, GST ilipanga kukusanya maduhuli ya Shilingi 350,000,000 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali. Vyanzo hivyo ni ada ya ushauri elekezi, tozo za ramani au machapisho ya jiosayansi na tozo za huduma za maabara. Hadi kufikia tarehe 31 Machi,
2018  GST  ilikuwa  imekusanya  jumla  ya  shilingi 294,700,000. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 84.2 ya lengo ililowekewa kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18.  
  1. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake, GST imepima na kuchora ramani za jiolojia na jiokemia za mfumo wa QDS kwa skeli ya 1:100,000 kwenye maeneo mapya (QDSs 264, 265) yaliyoko Wilaya ya Mahenge na Malinyi; na kufanya ugani (field checks) wa jiolojia na jiokemia ili kuboresha ramani 2 za QDS 64 na 65 za Wilaya ya Shinyanga. Vilevile, kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo, GST ilifanya tafiti mbalimbali za jiosayansi. Katika kipindi husika, GST kwa kushirikiana na Geological Survey of China ilifanya utafiti wa kina wa jiokemia katika maeneo ya Mbeya (QDS 244 na 245) na utafiti wa awali (Regional Scale Surveys) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar- es-Salaam na Morogoro (Tazama Picha Na.3), Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Mara kwa lengo la kutafuta madini mbalimbali. Kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani, GST ilikusanya taarifa na sampuli katika maeneo ya Wilaya za Kondoa na Chemba ili kupata vyanzo vya nishati ya joto ardhi kwa ajili ya maeneo ambayo yako mbali na gridi ya Taifa.
 
  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, GST na Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini ilisaini Hati ya Makubaliano kwa ajili ya kufanya utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kuainisha maeneo yenye uwepo wa madini kwenye maeneo ya Tunduma na Mtwara (QDS 257,
312, 313, 319, 320) yanayopakana na Zambia na Malawi. Aidha, GST ilitengeneza ramani mbalimbali za jiosayansi na kuzisambaza kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya Madini pamoja na matumizi mengine.   Picha Na. 3: Wataalam wa GST wakiendelea na kazi za Utafiti wa Jiolojia Mahenge.    
  1. Mheshimiwa Spika, GST iliendelea kuboresha huduma za maabara ambapo mfumo wa kompyuta kwa ajili ya kuratibu uchunguzi wa sampuli kwenye maabara uliandaliwa   na   kusimikwa   (Laboratory
  Information Management System - LIMS). Pia, GST imeendelea kutengeneza Internal Reference Standards za limestone, phosphate na dhahabu. Vilevile, GST ilifanya uchunguzi wa kemia, petrolojia, minerolojia, uchenjuaji  madini  na jioteknolojia  kwenye  sampuli 13,633 za miamba choronge, udongo na madini. Pia, vyungu (cupels) 4,558 na crucibles 4,626 vilitengenezwa kwa ajili ya kutumika kuyeyushia sampuli za dhahabu ambapo hapo awali vilikuwa vinanunuliwa nje ya nchi kwa gharama kubwa. Vilevile, GST ilifanya uchunguzi wa kimaabara wa jumla ya sampuli 361 za udongo, madini na miamba na taarifa zake ziliandaliwa ambapo ziliwasaidia wateja kupata vibali (export permits) vya kusafirisha sampuli nje ya nchi kwa uchunguzi zaidi. madini katika eneo la Itumbi – Chunya.Picha Na. 4: Wataalam wa GST wakifanya utafiti wa kina wa   Picha Na.5: Miamba Choronge – Diamond Drilling (DD) iliyotokana na kazi ya utafiti wa madini katika eneo la Itumbi – Chunya.   Picha Na.6: Uchorongaji kwa njia ya Diamond Drilling (DD) ukiendelea katika eneo la Itumbi - Chunya   Picha Na.7: Uchorongaji kwa njia ya Reverse Circulation (RC) ukiendelea katika eneo la Itumbi - Chunya  
  1. Mheshimiwa Spika, GST iliendelea na kazi ya kuratibu majanga asilia ya jiolojia ambapo takwimu kutoka vituo 8 vya kudumu vya kupimia matetemeko ya ardhi vilivyopo Dodoma, Mbeya, Arusha, Mtwara, Geita, Singida, Babati na Kibaya – Manyara zilikusanywa, kuchakatwa na kuhifadhiwa kwenye kanzidata. Kwa kutumia takwimu hizo, GST iliainisha maeneo yenye vitovu (epicentres) vya matetemeko na kuboresha ramani inayoonesha maeneo yenye vitovu vya matetemeko ya ardhi. Aidha, taarifa kuhusu matetemeko ya ardhi yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2017 hadi Machi, 2018 ilitolewa kwa wananchi na kwenye vyombo vya habari. Matukio hayo yameainishwa kwenye Jedwali Na.1.
 
  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, GST ilifanya utafiti
maalum wa kuangalia ubora na wingi wa madini ya   jasi katika maeneo ya Makanya na Bendera (Same), Mwanga (Mwanga), Itigi (Manyoni), Msagali (Mpwapwa) na Manda (Chamwino), Mpindiro, Mandawa, Mbaru, (Kilwa-Lindi) na Mkomole (Sumbawanga); utafiti maalum katika Wilaya ya Mufindi, Kijiji cha Isalavanu kwa maombi ya Serikali ya Wilaya ili kubaini uwepo wa madini yaliyofichwa katika maeneo hayo wakati wa Utawala wa Wajerumani kama ilivyokuwa inadhaniwa na wana kijiji hicho; utafiti wa jiosayansi ulifanyika katika mahandaki yaliyopo katika Kijiji cha Gibeshi Mkoani Simiyu ili kujua kama ni mahandaki ya asili au yamechimbwa na binadamu; utafiti wa jiosayansi katika  eneo  la  Nholi  -  Dodoma  ili  kubaini  chanzo na uwepo wa madini ya dhahabu katika eneo hilo; uchunguzi wa malikale katika Wilaya ya Same Kata ya Lugulu na Kitongoji cha Vumba pamoja na Mkoani Tanga katika Kata ya Pongwe; kukusanya taarifa za uwepo wa madini na utafiti wa miamba katika Mkoa wa Iringa, Wilaya za Mufindi, Iringa Vijijini na Kilolo; na pia GST ilishiriki katika ukaguzi wa taarifa zilizotumika kupata kiwango cha almasi kilichopo kwa sasa katika Mgodi wa almasi wa Mwadui na kuhakiki uwepo wa kiwango hicho cha almasi na kutoa mapendekezo kwa Serikali.  
  1. Mheshimiwa Spika, Pia, katika tafiti nyingi zilizofanywa na wataalam wa jiosayansi ya uchenjuaji zimebainisha kuwa madini mengi hubakia kwenye visusu (tailings) baada  ya  kuchenjuliwa.  Sababu za madini kubakia kwenye mabaki ni kutokana na kutofikiwa kwa kiwango cha ukubwa wa chembe (particle size) za mbale kinachotakiwa baada ya mwamba kuvunjwa na kusagwa; matumizi yasiyo sahihi ya kemikali zitumikazo kuchenjua na utumiaji wa vifaa visivyostahili.  Hii inatokana na wachimbaji
  wadogo kutofahamu tabia tofauti za miamba na mbale hivyo kupelekea kutotumia njia bora za uchenjuaji. Ni vyema wachimbaji wadogo wakafahamu njia bora za uchenjuaji kwa kufanya majaribio ya sampuli za mbale katika maabara mara kwa mara ili kutambua mtiririko mzuri, aina ya miamba, kiwango cha usagaji, njia na mbinu za uchenjuaji.  
  1. Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa wachimbaji wadogo, kama hawajui tabia za mbale ya sehemu wanayochimba, kabla ya kuanza uchenjuaji wapeleke sampuli za mbale (bulk samples) kwenye maabara za GST kwa ajili ya uchunguzi ili waweze kutambua njia bora za uchenjuaji. Lengo ni kupunguza madini kubaki kwenye visusu (tailings), kuongeza wingi wa uvunaji wa madini, kipato na faida kwa wachimbaji wa madini.
 
  1. Mheshimiwa Spika, GST  ilifanya  kazi  ya kuboresha Kanzidata ya jiosayansi na madini, ambapo jumla ya machapisho 412 yalibadilishwa kutoka katika mfumo wa karatasi na kwenda kwenye mfumo wa digitali; ramani 93 za jiosayansi zilikuwa ‘‘scanned’’ na kuhaririwa na kuwekwa kwenye mfumo wa utunzaji wa taarifa na machapisho (GMIS); Ramani 17 za jiolojia za mfumo wa QDS zimebadilishwa kutoka mfumo wa karatasi kwenda mfumo wa digitali (digitization) kwa lengo la kurahisisha usambazaji na utumiaji. Aidha, GST ilisambaza ramani na machapisho mbalimbali kwa wadau wa Sekta ya Madini kwa matumizi mbalimbali. Vilevile, GST imepokea na kuhakiki taarifa 205 kutoka kwa wamiliki wa leseni za utafutaji na uchimbaji madini kwa ajili ya kujua uhalisia wake na kuzitunza kama ilivyoelekezwa  kwenye  Sheria  ya  Madini  ya  Mwaka
2010 na Marekebisho yake ya Mwaka  2017.  
  1. Mheshimiwa Spika, GST ilifanya utafiti wa uchenjuaji mbale za madini ya dhahabu katika maeneo ya Londoni na Sambaru (Singida) kwa ajili ya kusaidia wachimbaji wadogo;   na   kukamilisha   uchakataji wa taarifa za awali za jiosayansi (Geotechnical and seismological) ili kuainisha maeneo hatarishi na salama kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika Jiji la Dodoma ikizingatiwa kuwa maeneo hayo yapo katika ukanda wa matetemeko ya ardhi. Aidha, GST ilitoa  ushauri  elekezi  wa  jiosayansi  kwa  kampuni
10 za utafutaji na uchimbaji madini ya metali na ya viwandani. GST pamoja na hayo ilipokea taarifa zenye jumla ya  leseni 247 za utafutaji madini (Prospecting licences),

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi