Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Hospitali Mirembe Yapokea Gari za Wagonjwa
Dec 08, 2023
Hospitali Mirembe Yapokea Gari za Wagonjwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule leo Desemba 8, 2023, akizindua gari mbili za Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe iliyopo katika Kata ya Hazina jijini Dodoma
Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule leo Desemba 8, 2023, amezindua gari mbili za Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe iliyopo katika Kata ya Hazina jijini Dodoma ambapo kwa kipindi kirefu hospitali hiyo imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa vitendea kazi.

Akizindua gari hizo ambazo moja ni kwa ajili ya kubebea wagonjwa na nyingine ni kwa matumizi ya kazi za kawaida za hospital, Mhe. Senyamule amesisitiza utunzaji wa gari hizo.

"Serikali ya Awamu ya Sita wakati huu imekuwa na kasi kubwa ya kuimarisha huduma za afya na kwa mkoa wetu wa Dodoma kila ngazi imeimarika kwa nafasi yake, kwa mwaka huu pekee kumekuwa na uzinduzi wa gari za wagonjwa ambapo mkoa wetu umepata jumla ya gari 30,  10 ni kwa ajili ya kazi na 20 kwa ajili ya kubeba wagonjwa”,

"Natoa shime kwa watumiaji wa gari hizi kuzitumia kwa utaratibu na miongozo ili ziweze kudumu kama ilivyotarajiwa, hivyo vitendea kazi hivi vitumike vizuri. Afya ya akili ni tatizo linalohitaji kushughulikiwa mapema ili lisikufikishe sehemu mbaya, huduma munayoitoa ikifikia watu wengi, itatengeneza utashi zaidi”, amefafanua Mhe. Senyamule.

Hata hivyo Mkurungenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mirembe, Dkt. Paul Lawala ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuleta vitendea kazi kwenye hospitali yake kwani hapo awali walikuwa wakipata changamoto kwenye utekelezaji wa huduma hasa linapohitajika suala la usafiri kwani kwa sasa wamepanua huduma za hospitali za dharura na mahututi hivyo ujio wa gari hizi umefika wakati muafaka wa kutatua changamoto hiyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi