Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

HESLB Yaongeza Muda wa Kuomba Mkopo Hadi Agosti 23
Aug 15, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46103" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuongeza muda wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao kwa siku tano hadi Ijumaa, Agosti 23, 2019 ili kuwapa fursa waombaji ambao hawajakamilisha maombi yao kutumia muda ulioongezwa kufanya hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru (pichani) amesema jijini Dar es salaam leo (Alhamisi, Agosti 15, 2019) kuwa HESLB ilianza kupokea maombi ya mkopo Julai 1 mwaka huu na tarehe ya mwisho ilikua Agosti 15, 2019.

Kwa mujibu wa Badru, HESLB imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji mikopo ambao hawajakamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nyaraka muhimu.

“Ingawa hadi leo (Agosti 15, 2019) tumeshapokea maombi zaidi 74,821 yaliyokamilika kwa njia ya mtandao, tumepokea pia maombi kutoka kwa wateja wetu wakitaka kuongezewa muda ili wakamilishe nyaraka muhimu kama nakala za vyeti vya vifo vya wazazi wao, barua kutoka kwa wadhamini wao na nyaraka nyinginezo … tumewasikiliza na kuongeza muda,” amesema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amewataka waombaji mkopo ambao hawajakamilisha maombi yao kutumia muda ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa HESLB haitaongeza muda zaidi baada ya tarehe 23 Agosti mwaka huu.

“Tunasihi waombaji wetu watumie muda huu ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa hatutaongeza tena. Baada ya Agosti 23, tutaanza kufanya uchambuzi wa maombi tuliyopokea ili tuwapangie mikopo wenye sifa kwa wakati na tupeleke fedha za mikopo vyuoni kabla vyuo havijafunguliwa,” amesema Badru.

Katika kipindi kilichoongezwa cha hadi Agosti 23, Badru amesema dawati la huduma kwa wateja la HESLB klitakuwa wazi ili kutoa ufafanuzi kwa waombaji mkopo pale utakapohitajika. Dawati hilo linapatikana kuanzia saa 2:30 asubuhi – saa 11:30 jioni kupitia:

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi