Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Halmashauri Nchini Zatakiwa Kuwa na Mikakati ya Mawasiliano
Aug 30, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34641" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Chamacha Mawasiliano Serikali (TAGCO) walipomtembelea ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha Tabora, Singida na Dodoma ikiwa ni jutekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikali kilichofanyika mapema mwezi machi mwaka 2018. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa, anayemfuati ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Sarah Kibonde Msika, mjumbe wa Kamati tendaji wa chama hicho Innocent Byarugaba na Mweka Hazina Msaidizi Gerald Chami.[/caption]

Na: Frank Shija – Idara ya Habari –MAELEZO, Singida

Halmashauri zote nchini zimetatikiwa kuwa na mkakati wa mawasiliano utakaotumikakufikisha taarifa za utekelezaji wa sshughuli za maendeleo kwa wananchi.

Wito huo umetolewa leo Wilayani Mkalama mkoani Singida na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bibi. Zainabu Kawawa  wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea changamoto zinazowakabili Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati  inayohusisha mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma.

[caption id="attachment_34642" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa, akimwelezea jambo Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani , Omari Mtamike walipomtembelea ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha Tabora, Singida na Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikali kilichofanyika mapema mwezi machi mwaka 2018. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Sarah Kibonde Msika.[/caption] [caption id="attachment_34643" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga akifafanua jambo mbele ya wageni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) walipomtembelea ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha Tabora, Singida na Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikali kilichofanyika mapema mwezi machi mwaka 2018. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Sarah Kibonde Msika na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa.[/caption]

Zamaradi amesema kuwa Halmashauri zinaowajibu wa kuajiri na kuwajengea uwezo Maafisa Habari ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuhabarisha jamii juu ya masuala ya maendeleo yanayofanywa na Serikali katika maeneo yao.

“Ni wajibu wetu sisi kama wataalamu wa mawasiliano kuhakikisha tunakuwa na mikakati amdhubuti ya mawasiliano katika Halmashauri zetu ili kufanyikisha utoaji wa taarifa kwa jamii juu ya namna ambavyo Serikali yetu inavyotekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo”, alisema Bibi. Zamaradi.

Aliongeza kuwa inasikitisha kuona baadhi ya Halmashauri nchini zinakosa kuwa na Maafisa Habari ambao wajibu wao ni kuhakikisha watanzania wanapata kujua nini Serikali yao inafanya katikati maeneo yao.

[caption id="attachment_34644" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja ujumbe kutoka Wizara ya Habaari, Utamadduni, Sanaa na Michezo pamoja na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) walipomtembelea ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha Tabora, Singida na Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikali kilichofanyika mapema mwezi machi mwaka 2018.[/caption]   [caption id="attachment_34646" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga (kushoto) na Mweka Hazina wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO), Gerald Chami mara baada ya kumaliza ziara ya ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamadduni, Sanaa na Michezo pamoja na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) leo. Ujumbe huo upo katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha Tabora, Singida na Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikali kilichofanyika mapema mwezi machi mwaka 2018.Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa. (Picha na: Idara ya Habari –MAELEZO, Singiida)[/caption]

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida Mhandisi Godfrey Sanga amesema kuwa habari ni suala muhimu sana katika ustawi wa jamii kutokana na ukweli kwamba bila mwananchi kupata taarifa juu ya nini Serikali yao inafanya wanakuwa kama wako gizani wakati ni ukweli kwamba yapo mengi ambayo Serikali yao inayafanya kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

“Niseme tu kuwa kwa sasa habari ni kama uti wa mgongo, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha wananchi wanapata habari za uhakika tena kwa wakati, kwa kutambua hilo katika Halmashauri yetu tuaendeleo kuhakikisha wananchi wanapata habari na tutamuwezesha Afisa Habari wetu kadri ya mahitaji yake” alisema Mhandisi Sanga.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Bibi. Sarah Msika amesema kuwa TAGCO kwa kutambua jukumu kubwa walilonalo wanachama wake kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamekuja na mkakati wa kutembelea Maafisa wa Habari maeneo yao ya kazi ili kujionea namna wanavyofanya kazi na kushauriana nao namna bora ya kuongeza ufanisi katika kazi zao.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na TAGCO wamekuwa katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kilichofanyika machi 12 hadi 16 mwaka huu mkoani Arusha ambapo mpaka sasa wamekwisha tembelea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma, Mtwara,Lindi, Tabora na Singida.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi