Filamu ya Royal Tour Yazinduliwa Jijini Dar es Salaam
May 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Picha ikionesha Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo uzinduzi wa Filamu ya ‘Tanzania The Royal Tour' unafanyika leo Mei 8, 2022. Katika uzinduzi huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atawaongoza viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi katika kushuhudia tukio hilo litakaloanza saa nane mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali (hawapo pichani) wakati akizindua filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi na wageni mbalimbali wakitazama filamu ya ‘Tanzania Royal Tour’ baada ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es Salaam