Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Filamu ya Royal Tour Yategemewa Kuleta Matunda
Apr 29, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff - ARUSHA

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali anayoiongoza imetangaza utalii na vivutio vya biashara kupitia filamu ya ‘Royal Tour’ jambo linalompa matumaini kwamba italeta manufaa kwa Taifa.

Mkuu wa Nchi ameyasema hayo leo jijini Arusha katika hafla ya kuzindua filamu hiyo kwenye jiji hilo la kitalii linalopatikana Kaskazini mwa Tanzania.

“Ni matumaini yetu kwamba hii filamu ya Royal Tour itakwenda kuleta matunda makubwa, mazuri na matamu kwa Tanzania,” ameeleza Rais Samia.

Pamoja na hilo, Mheshimiwa Rais amewaomba Watanzania kuiangalia filamu hiyo ili kujionea mambo mbalimbali yaliyopo nchini.

 “Yatakayooneshwa hapa pengine hata Watanzania hamuyajui, tuna ghala kubwa la siri linalohifadhi meno ya tembo na faru, tumelihifadhi na kulionesha kwenye filamu hiyo ili ulimwengu uone tulivyoteketeza wanyama,” amearifu Mkuu wa Nchi.

Rais Samia amewashukuru wananchi wote waliomuunga mkono kwa kuchanga fedha zilizofanikisha kurekodiwa na kuzinduliwa kwa filamu ya ‘Royal Tour’.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi