Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

EPZA, TCCIA Kushirikiana Kuhamasishaji Wawekezaji Wazawa
Apr 14, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30421" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA), James Maziku akielezea majukumu ya mamlaka hiyo mbele ya wajumbe wa Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA) walipofanya ziara katika mamlaka hiyo jana jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ililenga kuwajengea uwelewa wa pamoja ili kuhamasisha wazawa zaidi kuwekeza katika maeneo hayo.[/caption] [caption id="attachment_30422" align="aligncenter" width="561"] Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA), Nyanda Shuli akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) walipofanya ziara katika mamlaka hiyo jana jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ililenga kuwajengea uwelewa wa pamoja ili kuhamasisha wazawa zaidi kuwekeza katika maeneo hayo.Kushoto ni Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA Bi. Grace Lemunge.[/caption] [caption id="attachment_30423" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wajumbe kutoka Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA) wakati wa ziara katika mamlaka hiyo jana jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_30424" align="aligncenter" width="1000"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania, wilaya ya Ubungo Bw. Clement Bocco akimsikiliza Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd, Rigobert Massawe, walipotembelea kiwanda hichi ikiwa ni ziara yao ya kutembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA) Benjamin Mkapa EPZ Ubungo External jijini Dar es Salaam jana. Kiwanda hicho kinatengeneza nguo aina ya Jeans na kuziuza katika masoko ya nje.[/caption] [caption id="attachment_30425" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd wakiendelea na shughuli za ushonaji wa nguo ambaozo baadaye usafirishwa nje ya nchi. Kiwanda hicho kipo katika eneo la uwekezaji la Benjamin Mkapa EPZ, Ubungo External jijini Dar es Salaam yalipo Makao Makuu ya Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA).[/caption] [caption id="attachment_30426" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa za mazao ya nafaka Somani Agro Export Ltd (SAEL), Dkt. Alykhan Somani akielezea jinsi mazao hayo yanavyochakatwa katika madaraja tofauti tayari kwa kuuzwa nje ya nchi alipotembelewa na wajumbe wa Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) jana jijin Dar es Salaam. Wajumbe hao wa TCCIA walifanya ziara katika ofisi za Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA) kwa lengo la kujengewa uelewa na kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana.[/caption] [caption id="attachment_30427" align="aligncenter" width="1000"] Uwekezaji(EPZA) Bi. Grace Lemunge (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) mara baada ya kumaliza ziara yao katika Ofisi za mamlaka hiyo jana jijini Dar es Saalam.(Picha zote na: MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi