Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

EAC Yapiga Hatua Miundombinu ya Kimkakati- Ruto
Mar 07, 2026
EAC Yapiga Hatua Miundombinu ya Kimkakati- Ruto
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akipokea vitendea kazi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo aliyemaliza muda wake, Rais wa Kenya Mhe. William Somoei Ruto katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Jijini Arusha.
Na Na Timothy Mwakyenda - MAELEZO

Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Rais wa Kenya Mh.Dkt .William Ruto amesema jumuia hiyo imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayolenga kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ameyasema hayo leo machi 7 ,2026 wakati akifungua mkutano wa 25 wa kawaida wa wakuu wa inchi wa (EAC) Uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano Jijini Arusha (AICC).

Mwenyekiti Ruto alitolea mfano wa Reli ya kisasa ya umeme (SGR) ya nchini Tanzania kuwa ni moja ya mifano ya mafanikio ya uwekezaji wa miundombinu ndani ya ukanda huo.

"Hatua hiyo imeongeza ufanisi katika usafirisha wa bidhaa na kurahisisha biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki", Amesena Ruto.

Kwa mujibu wa takwimu  zilizotolewa , Reli hiyo ya kisasa iliyoanza kufanya kazi Juni 24, 2024 imekuwa ikisafirisha wastani wa abiria zaidi ya elfu kumi kwa siku kati ya Dar-es- salaam na Dodoma.

Aidha Ruto alieleza kuwa juhudi za kuimarisha usafiri wa majini katika ziwa  Viktoria umeaanza kuzaa matunda baada ya meli mpya za mizigo kuanza kufanya kazi katika ukanda huo, hali iliyoongeza uwezo wa kusafirisha mizigo hadi kufikia tani 890, 000 Kwa mwaka

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi