Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Tulia Afanya Kampeni za Urais wa IPU Nchini Angola
Oct 23, 2023
Dkt. Tulia Afanya Kampeni za Urais wa IPU Nchini Angola
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 23 Oktoba, 2023 akizungumza na Wajumbe wa kundi la Latini na Amerika kusini katika ukumbi mdogo wa Bunge la Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa IPU akiwaomba wampigie kura katika Uchaguzi wa Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 nchini humo.
Na Michael Msombe

Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifurahia jambo na Spika wa Seychelles, Mhe. Roger Mancienne (katikati) pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Zungu walipokutana katika Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Bunge la Angola uliopo Jijini Luanda nchini Angola leo tarehe 23 Oktoba, 2023. Dkt. Tulia anagombea nafasi ya Urais wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 nchini humo.

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati), akizungumza jambo na Spika wa Bunge la Namibi,  Mhe. Peter Katjavivi (kushoto) pamoja na Spika wa Bunge la Zambia, Mhe. Nelly Mutti (kulia) wakati walipokutana katika Ofisi ndogo za Bunge la Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ukiendelea nchini humo leo tarehe 23 Oktoba, 2023

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi