Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt Tizeba Afanya Mazungumzo na Watendaji Wakuu wa Taasisi ya Bill&Melinda Gates Foundation
Sep 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akifanya mazungumzo na Watendaji wakuu wa Taasisi ya Bill&Melinda Gates Foundation Jana tarehe 5 Septemba 2018 mjini Kigali Nchini Rwanda. (Picha Na Mathias Canal,WK)
Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akifanya mazungumzo na Watendaji wakuu wa Taasisi ya Bill&Melinda Gates Foundation Jana tarehe 5 Septemba 2018 mjini Kigali Nchini Rwanda.
Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifanya mazungumzo na Watendaji wakuu wa Taasisi ya Bill&Melinda Gates Foundation Jana tarehe 5 Septemba 2018 mjini Kigali Nchini Rwanda.
 
Na: Mathias Canal, Kigali-Rwanda
Waziri Wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba Jana tarehe 5 Septemba 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wakuu wa Taasisi ya Bill&Melinda Gates Foundation juu ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo nchini Tanzania hususani katika sekta ya kilimo pamoja na kuzungumzia Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kigali Conversion Centre mara baada ya kukamilika kwa siku ya kwanza ya ufunguzi wa kongamano la Mapinduzi ya Kijani barani Afrika (African Green Revolution Forum –AGRF) linalotuama kwa siku nne kuanzia tarehe 5-8 Septemba 2018.
Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Taasisi ya Kilimo Trust pamoja na Muwakilishi wa Benki ya Dunia katika bara la Afrika.
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi