Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, (Picha na Ikulu 28/10 /2017.)
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Syrus Castco (katikati) akisoma taarifa yake katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara hiyo katika Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani). Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) na Naibu Waziri Mhe. Shadya Mohamed Suleiman, (Picha na Ikulu. 24/10 /2017.)
Maafisa wa Idara zilizo chini ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,Vijana, Wanawake na Watoto wakiwa katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja na kuongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), (Picha na Ikulu 28/10 /2017.)