Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Ndumbaro Ashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola
Nov 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro anashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Mjini Balaclava, nchini Mauritius kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba, 2022.

Mkutano huo umefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritius, Mhe. Pravind Kumar Jugnauth.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali katika sekta ya sheria yakiwemo masuala ya upatikanaji haki, haki za binadamu, matumizi ya akili bandia katika mifumo ya Mahakama, umuhimu wa sekta ya sheria katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Mambo mengine yanayotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Urejeshwaji wa Wahalifu, Mikataba ya Uwekezaji, Hatua zilizochokuliwa na Nchi Wanachama katika maeneo mbalimbali yakiwemo Mapambano Dhidi ya Rushwa, Sheria za Kudhibiti Uhalifu wa Mtandao, Ushirikiano katika masuala ya Jinai na Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala na  wajibu wa Vyombo vya Habari katika kutekeleza Haki ya Kutoa Maoni.

Mkutano huo unahudhuriwa na Mataifa zaidi ya 30 kutoka katika Wanachama wa Jumuiya ya Madola Duniani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi