Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Nchemba Akutana na Kuzungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi La Magereza
Nov 30, -0001
Dkt. Nchemba Akutana na Kuzungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi La Magereza
Kikao kikiendelea kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu ambaye alifika ofisi za Hazina Jijini Dodoma kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuliongoza Jeshi hilo hivi karibuni.
Na Josephine Majura WF, Dodoma

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa kikao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu ambaye alifika ofisini kwake kujitambulisha jijini Dodoma, ambapo walitumia fursa hiyo kujadili mipango ya maendeleo ya Jeshi hilo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, ambaye amefika ofisini kwake kujitambulisha, akiwa ameambatana na Maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya namna ya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa majukumu ya Jeshi hilo yanatekelezwa kwa ufanisi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye alifika ofisi za Hazina Jijini Dodoma kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuliongoza Jeshi la Magereza, hivi karibuni.
 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi