Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Mwigulu Ateta na Mkurugenzi wa Citi Bank
Nov 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho


Scola Malinga na Josephine Majura, DSM


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwingulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka CITI Bank unaosimamia Ukanda wa  Jangwa la Sahara na Mashariki ya Kati , ambapo benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji na kufanya tathimini ya  uwezo wa`nanchi kukopesheka (credit rating).


Dkt. Nchemba amefanya kikao jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group, Bw. David McD. Livingstone amesema Benki yake inajivunia kufanya kazi na Tanzania katika kufikia agenda yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Mhe. Dkt. Nchemba. alielezea kuwa wamejadiliana namna ya kuharakisha ukamilishaji wa suala la tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka katika masoko ya kimataifa (credit rating) ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo CITI Group ndio  washauri wakuu wa zoezi hilo. 


Alisema kuwa Serikali inaendelea kujadili na kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi mingine ambayo wao wanahusika moja kwa moja kama vile mradi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na miradi mingine ya maendeleo ambayo Serikali iliwahusisha katika utafutaji wa fedha ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.


Dkt. Nchemba alisema kuwa jambo la kuendeleza ushirikiano katika masuala ya kitaalamu hasa hilo la creding rating pamoja na masuala ya uhamasishaji wa upatikanaji wa rasilimali fedha ambazo Serikali inazipata  kutoka Taasisi mbalimbali za fedha Benki kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) pamoja na miradi mingine ya maendeleo.


“Tumekubaliana pia katika mazungumzo yetu kwamba wasimamie wito uliotolewa na Mhe. Rais ya kuwaalika wawekezaji kama vile taasisi za kifedha na sekta binafsi kwa kuwa wana mtandao mkubwa katika maeneo tofauti tofauti ili  waje wawekeze na kutumia fursa zilizopo nchini hususan utengenezaji bidhaa ambazo zimepanda bei kama mafuta ya kula, mbolea pamoja na unga wa ngano”, alisema Dkt. Nchemba.


Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group, Bw. David McD. Livingstone amekukubali kuendelea kushirikiana na Serikali kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo na pia kukamilisha zoezi la kutathimini na  kuangalia uwezo wa nchi kuweza kukopa na kulipa madeni na kuhakikisha kwamba zoezi hilo linakamilika ndani ya muda uliopangwa na kuhamasisha uwekezaji kutoka Sekta Binafsi ili waweze kuchangia maendeleo ya nchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi