[caption id="attachment_36125" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na wadau wa mchezo wa Kriketi alipokutana nao hapo jana katikati ukumbi wa mkutano uliopo Uwanja wa Taifa, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo.[/caption]
Na Lorietha Laurence - WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wiki mbili kwa vilabu vyote vya mchezo wa Kriketi nchini ambavyo havijasajiliwa kufika Baraza la Michezo La Taifa kwa ajili ya kujisajili .
Akizungumza na wadau hao wa mchezo huo jana katika Ukimbi wa mikutano uliopo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa ni wajibu wa kila kilabu cha mchezo nchini kufuata sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya michezo.
“Kama kuna kilabu chochote cha mchezo wa kikreti kipo na hakijasajiliwa, natoa wiki mbili kuweza kufuata taratibu na sheria za usajili ili viweze kutambulika kisheria ” alisema Dkt. Mwakyembe.
[caption id="attachment_36127" align="aligncenter" width="800"] Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge (kulia) akizungumza na wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto).[/caption]Aidha aliongeza kwa kuutaka uongozi wa Chama cha Kriketi Tanzania kuhakikisha unatenga siku moja kwa ajili ya mkutano na wanachama wake ili kupata nafasi ya kupitia vipengele vinavyounda katiba ya chama hicho kwa ajili ya maboresho mbalimbali.
Vilevile Waziri Dkt. Mwakyembe alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali zinazokikabili chama hicho cha mchezo wa Kriketi na kuhaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Kwa Upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Makoye Nkenyenge amewataka wanachama hao kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Dkt. Mwakyembe kwa kuhakikisha wanasajili vilabu vyote ambavyo havijasajiliwa.
[caption id="attachment_36128" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kushoto) akieleza jambo kwa wadau wa chama cha kriketi Tanzania walipokutana nao jana uwanja wa Taifa wa Michezo, katikati ni Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Makoye Nkenyenge.[/caption] [caption id="attachment_36126" align="aligncenter" width="800"] Wadau na wanachama wa chama cha Kriketi Tanzania wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea baina yao na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika Picha), katika kikao kilichofanyika jana uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.[/caption]Naye Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania Bw. Taher Kitisa ameahidi kushirikiana na wanachama wenzake katika kuhakikisha wanapitia katiba ya chama hicho na kuifanyia maboresho.
Dkt. Mwakyembe alikutana na wanachama wa Kriketi zaidi ya 60 lengo ikiwa ni kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu mchezo huo ikiwemo uboreshwaji wa uongozi wa chama hicho kwa manufaa ya ustawi wa mchezo huo.