Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Madeni Aendesha Operesheni Maalum ya Ukusanyaji Mapato Jiji la Arusha
Sep 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni (kulia) akiongozana na mmoja wa  Watendaji wa Halmashauri ya Jiji hilo wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko Kuu la Jiji hilo wakati wa ziara yake aliyoifanya jana (Jumatatu Septemba 10, 2018).[/caption]   [caption id="attachment_35121" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni (wa pili kulia) akitazama moja ya mizani inayotumiwa na Wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali katika Jiji hilo wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko Kuu la Jiji hilo jana (Jumatatu Septemba 10, 2018).[/caption]

Na. Fatuma Ibrahimu, ARUSHA JIJI

MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni amezindua operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ya Jiji la Arusha kwa Wafanyabiashara wote Jijini humo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuwahamasisha Watanzania kulipa kodi.

Akizundua operesheni  hiyo jana Jijini Arusha (Jumatatu Septemba 10, 2018), Dkt. Madeni alisema operesheni hiyo imelenga kuhakikisha kuwa kila  mfanyabiashara katika Jiji hilo analipa kodi ili kuwawezesha  wananchi wa kipato cha chini  kupata huduma bora za kijamii ikiwemo  maji, afya na elimu.

Aidha Dkt. Madeni amembadilishia nafasi ya kazi msimamizi wa Soko Kuu katika Jiji hilo, Bw. John Ruzga  kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo mapato ya halmashauri kutokana na soko hilo kukusanya Tsh. Milioni 23 kwa mwezi badala ya la lengo lililokusudiwa la Tsh 31.6 kwa mwezi na Halmashauri ya Jiji hilo.

[caption id="attachment_35123" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Arusha (kulia) akizungumza na mmoja wa Wafanyabiashara wa matunda katika Soko Kuu la Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua vyanzo mbalimbali vya mapato katika Soko hilo hapo jana (Jumatatu Septemba 10, 2018) ambapo aliambatana na timu ya watendaji  wa Halmashauri ya Jiji hilo.[/caption]

“Nimebaini changamoto zilizosababishwa na msimamizi wa soko hili ikiwemo ni pamoja na wamiliki wa vibanda na vizimba kukodosha wafanyabiashara wengine kinyumbe na utaratibu” alisema Dkt. Madeni.

Dkt. Madeni alisema kuwa operesheni hiyo ni endelevu na hivyo aliwataka Watendaji mbalimbali katika Jiji hilo kuhakikisha kuwa operesheni hiyo inafanikiwa ili kuiwezesha Halmashauri hiyo kufikia malengo iliyojiwekea.

Kwa mujibu wa Dkt. Madeni alisema Ofisi yake pia imekusudia kufanya ziara katika masoko na vyanzo vyote vya mapato vilivyo chini ya halmashauri ya Jiji hilo ili kuhakikisha wafanyabiashara wote na wamiliki wa vibanda wana leseni za muda husika, risiti halali za kodi  na mikataba halali ya halmashauri hiyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi