Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Jafo: Utatuzi Changamoto za Muungano Haujapoa
Oct 17, 2023
Dkt. Jafo: Utatuzi Changamoto za Muungano Haujapoa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu utatuzi wa changamoto za Muungano kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali inaendelea kujadili na kutatua changamoto za Muungano zinazojitokeza

Amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu utatuzi wa changamoto za Muungano kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia vikao vyake mwaka 2006, hoja 25 zimejadiliwa na hadi sasa hoja 22 zimepatiwa ufumbuzi na kuondolewa kwenye orodha ya Hoja za Muungano.

Amebainisha kuwa mwaka 2010 hoja mbili zilipatiwa ufumbuzi, mwaka 2020 hoja tano zilipatiwa ufumbuzi, mwaka 2021 hoja 11 zilipatiwa ufumbuzi na mwaka 2022 hoja nne zilipatiwa ufumbuzi.

Aidha, Waziri Jafo amebainisha kuwa hoja nne zilizobaki ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ili kufikia lengo la kuzipatia ufumbuzi na kuziondoa katika orodha ya Hoja za Muungano.

 

Kutokana na hatua hiyo Waziri Dkt. Jafo ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Serikali zote mbili yaani SJMT na SMZ kwa nia yake ya dhati ya kutatua changamoto za Muungano.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi