Na Beatrice Lyimo - CHINA
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ataendelea na ziara yake nchini China ambapo leo Ijumaa mchana atatembelea Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari cha China na kutoa mhadhara.
Katika mkutano huo, moja ya masuala anayotarajia kuzungumza na wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho ni kuhusu diplomasia ya Tanzania na China iliyopelekea kuwa na ushirikiano wa karibu mpaka sasa.
Aidha, Dkt. Abbasi pia atazungumzia wajibu wa wanahabari na namna wanavyotakiwa kuenenda ili kutekeleza wajibu wao katika sekta nzima ya habari na mawasiliano.
Mbali na hayo, akiwa msimamizi wa sekta ya habari nchini Tanzania Dkt. Abbas katika mkutano huo ataeleza hali ya sekta ya habari Tanzania ilivyo sasa na ijayo kwa maendeleo ya nchi.
Dkt. Abbasi na ujumbe wake wa Maafisa Habari na Uhusiano Serikalini wapo mjini Beijing kwa ziara iliyolenga kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano.