Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dhana ya Maendeleo ya Watu na Vitu Yafafanuliwa
Jun 17, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51619" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.(Picha kutoka Maktaba)[/caption]

Na Frank Mvungi, Dodoma

Dhana ya maendeleo ya vitu na watu imekuwa jambo linaloleta mkanganyika kwa baadhi ya watu na kuamua kwa makusudi kupotosha dhamira safi ya Serikali kuwekeza katika vitu vinavyoonekana na kushikika ili kuchochea ustawi wa wananchi .

Kwa muktadha huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi aliguswa na kuamua kueleza kuhusu dhana hii kwa kueleza kuwa maendeleo ya watu yanategemea maendeleo ya vitu ikiwemo miundombinu kama ya Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano na pia ujenzi wa Hospitali na Vituo vya Afya.

Utaona Serikali inapotekeleza mradi kama huu wa SGR unaogharimu takribani  Trilioni  7 wananchi wanapewa ajira, wanapata kipato, ujuzi na pia wataweza sasa kuboresha maisha yao kupitia kipato wanachopata kwa kujenga nyumba bora, kupanua wigo wa shughuli  za kiuchumi.

Kwa upande wa  hospitali  si tu zitasaidia upatikanaji wa huduma bora za afya,bali ajira zaidi ya 8000 zimetolewa kwa watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo wauguzi, madaktari, wafamasia na wataalamu wengine wakiwemo wa maabara, katika ujenzi utaona kuwa wananchi wa maeneo husika walipata ajira na hivyo kuwawezesha kukuza ujuzi wao na kukuza uchumi wa eneo husika.

Pia kujengwa kwa hospitali hizi kumewasaidia wananchi kupata huduma hizi katika maeneo yao na hivyo kupunguza muda waliokuwa wanatumia kufuata huduma katika maeneo ya mbali kabla ya uwekezaji huu uliofanywa na Serikali kwa ujenga Hospitali za Rufaa za mikoa 10, Wilaya 71, Vituo vya Afya 487.

Katika sekta ya Viwanda utaona mkazo uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano umewezesha viwanda zaidi ya 8000 kuanzishwa na vimetoa ajira kwa wananchi zaidi ya 200,000/ hali inayochangia katika kukuza uchumi na kuwezesha wananchi kupata bidhaa zenye ubora kutoka viwanda vya ndani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi