[caption id="attachment_35625" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akimsikilza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka wakati wa Kongamano la pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali wakiwemo wanafunzi na Watafiti.[/caption]
Na Beatrice Lyimo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali katika sekta ya afya kuleta matokeo chanya yanayokusudiwa na Serikali.
Dkt Ndugulile ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Pili la Tathmini na Ufutiliaji lililloandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Calfonia cha Marekani likilenga kujadili na kuweka mikakati ya namna bora ya kutumia matokeo ya tafiti za sekta ya afya kufanya tathmini na ufuatiliaji ili kuimarisha huduma zinazotolewa.
"Tuhakikishe rasilimali fedha inayowekezwa katika sekta ya afya inatumika vizuri ili kuleta matokeo chanya yanayotarajiwa na pia mfanye taafiti zitakazo saidia kuboresha na kusimamia sera na maamuzi ya Serikali" ameongeza Dkt. Ndugulile.
[caption id="attachment_35626" align="aligncenter" width="900"] Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka akizungumzia nafasi ya Chuo Kikuu Mzumbe katika kufanikisha programu mbalimbali za tafiti hasa katika sekta ya afya na kuzichakata taarifa zinazokusanywa ili zisaidie watunga sera katika kufanya maamuzi.[/caption] [caption id="attachment_35627" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikisha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Watafiti.[/caption]Aidha, Dkt Ndugulile, amekiasa Chuo hicho kufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wadau mbalimbali wanayojishughulisha na masuala ya afya kwa lengo la kuibua changamoto na kufanya utafiti ili kutoa majibu ambayo Serikali na wadau wanayahitaji ili kutoa majawabu kwa kuchukua hatua stahiki.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kupeana uzoefu kuhusu umuhimu wa ufuatiliaji na tathimini katika sekta ya afya.
"Chuo Kikuu Mzumbe kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa elimu na mafunzo katika eneo la ufuatiliaji na tathimini katika sekta ya afya ambapo kwa sasa tunaprogramu mbili za shahada ya kwanza na uzamili katika masuala ya afya na pia tunatoa kozi fupi fupi kwa ajili ya kujenga uwezo wafanyakazi katika sekta ya afya wanaoshughulika na mfumo" ameongeza Prof. Kusiluka
Aidha amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kimekuwa kikishirikiana na Wizara ya Afya , TAMISEMI na Chuo Kikuu cha Calfonia cha Marekani katika kujenga uwezo kwa wananfunzi wa Chuo hicho na wafanyakazi wanaotoa huduma katiika sekta ya afya.
[caption id="attachment_35628" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Pili la Ufuatiliaji na Tathmini linalofanyika Jijini Dodoma likishirikiasha wadau mabalimbali waliwemo wanafunzi na Watafiti.[/caption]