[caption id="attachment_47770" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.[/caption]
Na Mwandishi wetu – WHUSM,Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo amesema kuwa Bonanza la Michezo litaendelea kufanyika kila baada ya miezi miwili na litahusisha michezo mbalimbali.
Bw.Singo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipozungumza wakati akishukuru Watumishi wa Serikali na wananchi wa Jijini la Dodoma waliojitokeza kushiriki Bonanza hilo.
[caption id="attachment_47771" align="aligncenter" width="1000"]“Bonanza hili litafanyika kila baada ya miezi miwili lengo ikiwa ni kuimarisha afya zetu pamoja na kuimarisha upendo,amani na mshikamano tulionao Tanzania”alisema Bw.Singo.
Aidha Bw.Singo amesema kuwa Bonanza hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mbio za taratibu,mazoezi ya viungo, mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na michezo mingine.
Naye Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Daudi Manongi amesema kuwa Bonanza hilo limekuwa na faida nyingi kwani limewakutunisha Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Jiji la Dodoma katika kuimarisha afya zao na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza kazi zao.
Katika bonanza hilo timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya habari,Elimu na timu ya Joggin kutoka Dodoma ziliibuka washindi ,huku timu ya mpira wa miguu ya Serikali ikiifunga magoli matatu timu ya Boabao Queens ya Jiji la Dodoma iliyoambulia goli moja.