Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imekabidhiwa rasmi vitendea kazi vyenye umuhimu zaidi ili iweze kuanza kazi rasmI.
Akizungumza leo jijini Dodoma mara baada ya makabidhiano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ndg. Mohammed Khamis Abdulla amesema tume hiyo itaanza kazi Januari 2024.
"Leo tumekabidhiana sheria na tumekabidhiana kanuni mbili, hizi ni nyenzo zitakazoiwezesha tume hiyo kuanza kazi rasmi," ameeleza Ndg. Abdulla.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Adadi Rajabu amefahamisha kuwa nchi jirani tayari zina tume kama hiyo hivyo Watanzania walikuwa wakisubiria kwa hamu kuanzishwa kwa tume hiyo.