Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 90.7 Zalipa Madai ya Watumishi 65391
Jan 31, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Daudi Manongi - PWANI

Serikali imelipa madai ya watumishi 65,391 yenye jumla ya Shilingi Bilioni 90.7

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa ya Serikali kupitia vyombo vya habari Kibaha, Pwani.

“Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na Watumishi wa Umma na inawapongeza kwa kufanya kazi kwa uzalendo na kwa kujitoa kwa dhati. Tunatambua kumekuwa na changamoto ya muda mrefu juu kuhusu upandishaji madaraja, miundo na madai ya malimbikizo”, amesema Msigwa.

Amefafanua kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan haijalala juu ya masuala mbalimbali ya watumishi.

Katika upande wa upandishaji vyeo Watumishi wa Umma, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imepandisha vyeo watumishi 190,562 na jumla ya gharama iliyotumika katika mishahara ya watumishi hao ni Shilingi Bilioni 39.6

Katika upande wa ulipaji malimbikizo ya watumishi, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya Watumishi wa Umma ambapo kuanzia mwezi Machi, 2021 hadi mwezi Januari, 2022 Serikali imelipa madai ya watumishi 65,391 yenye jumla ya Shilingi Bilioni 90.7

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi