Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 408.3 za TIB Zawanufaisha Wananchi
Mar 20, 2025
Bilioni 408.3 za TIB Zawanufaisha Wananchi
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bi. Lilian Mbassy akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.
Na Frank Mvungi, Dodoma

Benki ya Maendeleo TIB imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 408.3 katika miradi ya maendeleo kwenye sekta zinazogusa wananchi.

Akieleza mafanikio katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Machi 20, 2025, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Lilian Mbassy amesema, kati ya uwekezaji uliofanyika ni kwenye mifuko 9 yenye thamani ya shilingi bilioni 222.

"Kupitia uwekezaji huu, zaidi ya ajira mpya 12,547 zimezalishwa kutokana na benki kufadhili miradi ya maendeleo ya muda wa kati na mrefu nchini", alisisitiza Bi. Mbassy

Akifafanua amesema, TIB itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha mazingira ya uwekezaji wa moja kwa moja wa ndani na nje kwa maendeleo ya wananchi na ustawi wa kiuchumi wa Tanzania.

Mwelekeo wa TIB ni kuwekeza kwenye miradi ya ujenzi wa Makazi, Elimu, Utalii, Afya na Upanuzi wa Bandari Kavu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi