Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bilioni 30 Zatumika Ujenzi wa Hospitali za Kanda
Aug 31, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46383" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali.[/caption]

Na; Mwandishi Wetu

Takribani Shilingi Bilioni 30 zimetumiwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Kanda ili kuimarisha huduma za Afya hapa nchini ikiwa ni kusogeza zaidi huduma kwa wananchi.

Akizungumzia utekelezaji wa Serikali katika sekta ya Afya hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa (RHH) na sehemu kubwa ya ujenzi umekamilika.

“Niwathibitishie Watanzania kuwa azma yetu ya kuiendeleza nchi kwa kasi chini ya Jemedari Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kushika kasi na katika hili hakuna atakayetuzuia wala kuturudisha nyuma,” Amesisitiza Dkt Abbasi.

Alifafanua kuwa Hospitali hizi za Kanda zinajengwa katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Njombe, Songwe, Katavi, Geita na Dar es Salaam (Mwananyamala) nakuongeza kuwa SShilingi Bilioni 3 zimetolewa kujenga Hospitali ya Kanda ya Wazazi Mbeya na shilingi bilioni 6.32 kujenga Hospitali ya Kanda Mtwara.

Dkt. Abbasi aliongeza kuwa, katika kuwekeza kwenye maisha ya watu wa ngazi ya chini, Serikali mapema mwaka huu ilitoa shilingi Bilioni 105 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 ambapo katika miaka zaidi ya 50 ya Uhuru tumekuwa na Hospitali katika Wilaya 77 tu; ndani ya mwaka huu mmoja zinajengwa 67 ambapo ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.

Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini kwa kuimarisha huduma katika vituo vya afya, Zahanati, Hospitali za Wilaya na Kanda.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi