Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Bil. 922 Kuboresha Bandari ya Dar es Salaam.
Jul 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4999" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.(Picha na: Frank Shija)[/caption]

Na: Lilian Lundo

Jumla ya shilingi bilioni 922 zitatumika kwa ajili ya kuboresha bandari ya Dar es Salaam ili kuifanya kuwa ya kisasa itakayoweza kupokea meli na shehena kubwa za mizigo kwa wakati mmoja.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo leo katika eneo la bandari ya Dar es Salaam alipokuwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa bandari hiyo.

. [caption id="attachment_5002" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania Bi. Bella Bird na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge Mhe. Hawa Ghasia.[/caption] [caption id="attachment_5005" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),Mhandisi Deusdedith Kakoko kuhusu mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.[/caption]

“Mradi huu utakapokamilika utainufaisha Taifa letu na nchi jirani kama vile Malawi, Zambia, Kongo, Rwanda, Uganda na Burundi ambazo zinategemea bandari yetu kusafirisha mizigo,” amesema Dkt. Magufuli.

Amesema kuwa, bandari hiyo ni lango kuu la biashara na ni kitovu cha uchumi wa nchi. Hivyo kama itaboreshwa ufanisi na uwezo wake itasaidia kukuza uchumi wa nchi kuelekea uchumi wa kati.

Aidha amesema, uboreshaji wa bandari hiyo utaondoa ucheleweshaji wa upakuaji na upakiaji wa mizigo uliokuwa ukisababishwa na ufinyu wa gati lakini baada ya kukamilika kwa upanuzi huo meli kubwa zaidi zitaweza kutia nanga.

[caption id="attachment_5008" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Duniz Tanzania Bi. Bella Bird wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika leo bandarini hapo. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke na Waziri ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.[/caption] [caption id="attachment_5009" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.[/caption]

“Mradi huu ukikamnilika utaifanya badari ya Dar es Saalam kuwa ya mfano na kutakuwa hakuna ucheleweshaji wa mizigo na itachangia maendeleo kiuchumi sio tu kwa Tanzania bali hata kwa zile nchi zitakazokuwa zinatumia bandari hii kupitisha mizigo yao” alieleza Rais Magufuli.

Aidha Rais aliuataka wa TPA kuimarisha ulinzi katika badari hiyo ili mkuifanya kuwa mahali salama pa kupitishia mizigo na kuhakikisha mizigo yote inayopita bandarini taarifa zake zinajulikana.

  [caption id="attachment_5010" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Miundombinu Profesa Norman Sigalla walipokutana katika hafla ya uwekeaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_5011" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndungulile wakati wa hafla ya uwekeaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam leo.[/caption]

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa mradi huo utanufaisha Taifa la Tanzania pamoja na nchi jirani zinazotumia bandari hiyo.

“Mradi utabadilisha ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam na kuifanya kuwa ya kisasa,” amesema Prof. Mbarawa.

Nae Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kuwa uboreshaji wa bandari hiyo utaweza kuhudumia shehena ya mizigo kutoka tani milioni 14 zinazohudumiwa kwa sasa hadi kufikia tani milioni 28 na pia itaweza kuhudumia meli kubwa zenye urefu wa hadi mita 320.

[caption id="attachment_5014" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Bella Bird wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_5017" align="aligncenter" width="750"] Kikundi cha Vijana kutoka Kigamboni wakitumbuiza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam leo.[/caption] [caption id="attachment_5020" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa watumiaji wakubwa wa Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam leo. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania, Bella Bird amesema Benki hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) itaendelea kusaidia kukua kwa Tanzania na kusaidia kuboresha maisha Tanzania.

Katika Uboreshaji wa bandari hiyo, Serikali ya Tanzania inachangia dola milioni 63.4, Benki ya Dunia Dola milioni  345.2 na Serikali ya Uingereza Dola milioni 12.4. Mradi unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 36 chini ya kampuni ya China Harbour Engineering.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi