Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Benki ya Credit Suisse Kuipatia Tanzania Mkopo wa Sh. Bilioni 450
Jul 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Credit Suisse ya nchini Uingereza imeonesha nia ya  kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa zaidi ya Dola milioni 200 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi mikubwa ya Nishati ya Umeme na miundombinu ya Reli.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam katika Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Ujumbe wa  Benki ya Credit Suisse  ya Uingereza  ulioongozwa  na Mkurugenzi Mkuu  wa Benki hiyo Bw. Lawrence B. Fletcher,  kuhusu ushirikiano katika miradi ya maendeleo.

Dkt. Mpango alisema kuwa tayari zipo hatua mbalimbalimbali zimefikiwa katika kufanikisha upatikanaji wa Mkopo kutoka Benki ya Suisse hivyo kuwa na tumaini la kupata kiasi cha Dola milioni 2000 katika mwaka wa fedha wa 2018/19 .

“Miradi ya Kipaumbele ambayo Serikali inaitekeleza ni pamoja na Ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), kufufua Shirika la Ndege Tanzania kwa kununua Ndege mpya na miradi ya umeme ambayo itachochea maendeleo ya watu na Taifa kwa ujumla”, alieleza Dkt. Mpango.

Aliitaja miradi mingine ambayo Serikali inampango wa kuitekeleza kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Rufiji Haydro Project) ambalo kukamilika kwake kutasaidia kuzalisha umeme wa Megawati 2100 ambao utatumika katika kuchochea uchumi wa viwanda unaohitaji umeme wakutosha.

Waziri Mpango amebainisha kuwa Serikali inatekeleza miradi ya kupanua Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Kigoma pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara ambazo zitahudumia nchi ya Tanzania na nchi jirani ya Rwanda na Burundi hivyo kuchochea maendeleo.

Ameishukuru Benki ya Suisse, kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Maji, barabara na Umeme na kuahidi kuendelea kukuza ushirikiano na Benki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu  wa Benki ya  Credit Suisse ya nchini Uingereza,  Bw. Lawrence B. Fletcher,  amesema kuwa Benki yake inaangalia uwezekano wa kufadhili miradi  ya kipaumbele  ya Serikali ili kuweza kufanikisha nia yake ya kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Aidha amesema Benki yake itatoa mkopo wa  Dola milioni  200 baada ya hatua za mkopo huo kukamilika katika mwaka huu wa fedha ili kuweza kufanikisha kutekeleza miradi mbalimbali lakini pia ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano kati ya Benki yake na Tanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi