Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Benki Kuu ya Tanzania Yasajili Kampuni ya Kutoa Mikopo ya Nyumba
Aug 18, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na:  Mwandishi Wetu – Maelezo

Benki Kuu ya Tanzania imetoa leseni kwa kampuni mpya ya kutoa mikopo ya nyumba inayoitwa “First Housing Company (Tanzania) Limited”.

Taarifa iliyotolewa Jijini Dar es Salaam leo na Idara ya Sera na Leseni katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki ya Benki Kuu ya Tanzania, imeeleza kwamba leseni hiyo inaipa nafasi kampuni hiyo mpya kufanya biashara ya kutoa mikopo ya nyumba nchini.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo Makao makuu ya kampuni hiyo yatakuwa Jijini Dar es Salaam.Hii ni mara ya kwanza kwa Benki Kuu kutoa leseni kwa kampuni ya mikopo ya nyumba nchini.

Benki Kuu pia inatoa leseni na kusimamia benki, taasisi za fedha, maduka ya kubadilisha fedha, kampuni za karadha na zinazotunza kumbukumbu za ukopaji za wananchi (credit reference bureaus).

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi