[caption id="attachment_51055" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhuhu bidhaa za kiwanda cha vifaa vya umeme cha Africab Jijini Dar es Salaam kinachozalisha vifaa mbalimbali ikiwemo transfoma, katika mwendelezo wa Ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam[/caption]
[caption id="attachment_51056" align="aligncenter" width="750"]
Baadhi ya Vifaa vya Umeme vinavyozalishwa na kiwanda cha Africab kilichopo Jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma na nyaya za umeme.[/caption]
Na. Eric Msuya
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wadau wa Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kutoa ajira katika viwanda vidogo na vikubwa ili kupunguza adha ya ukosefu wa ajira kwa vijana Nchini.
Ameyasema hayo leo Jumatano katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Viwanda vilivyopo Jijini Dar es salaam na kutoa rai kwa kwa watanzania kutumia bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ili kuongeza ajira kwa vijana
[caption id="attachment_51057" align="aligncenter" width="750"]“Hongereni kwa kumuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa kuwapa ajira watanzania 150, ambao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali hapa nchini, lakini hata wale walikuwa nyumbani wamekaa bila kazi” alisema Mhe. Bashungwa
Katika Ziara hiyo Mhe. Bashungwa amewapongeza Bwana Charles Mlawa na Aloyce Ngowi ambao ni wamiliki wazawa wa kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kinachozalisha Vifaa vya Umeme (Soketi na Transfoma) hapa Nchini kwa lengo la kuunga mkono Serikali kufikia Uchumi wa kati wenye viwanda.
[caption id="attachment_51059" align="aligncenter" width="750"]“Nyie ni wazalendo, ni mfano tosha kwa wawekezaji wazawa kwa kufahamu umuhimu wa Serikali kufikia uchumi wa kati, transfoma na nyanya za kupitishia umeme zote zenye ubora sasa zinatengenezwa Tanzania tena mwenge, Dar es Salaam, na sio tena kuagiza kutoka nje ya Nchi” alisema Mhe. Bashungwa
aidha Mhe. Bashungwa alitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta ya Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono kwa kununua bidhaa za ndani zinazo tengenezwa na wawekezaji wazawa na wazalendo
[caption id="attachment_51062" align="aligncenter" width="750"]“Niwaombe watanzania kuendelea kuipa kipaumbele neno ‘MADE IN TANZANIA’ utajisikiaje umeenda Nchi za watu ukakuta chombo unachotumia kimewekwa nembo ya Tanzania, hakika ni fahari sana” alisema Mhe. Bashungwa
Naye Mkurugunzi Mkuu wa kiwanda cha Tropical, Ndugu Charles Mlawa ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwaunga mkono na kuwajali katika kuhakikisha sera na lengo la kufikia uchumi wa kati Nchini ifikapo 2025, kwani mpaka sasa kiwanda hicho kinapata umeme wa uhakika kutoka Tanesco.
“Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuendelea kutuunga mkono sisi wawekezaji wa ndani, kwetu sisi ni fahari na tutaendelea kuiunga mkono Serikali yetu” alisema Bwan. Mlawa
Waziri Bashungwa katika ziara yake, pia alitembelea kiwanda cha AFRICAB kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kinacho jihusisha na utenegezaji wa vifaa vya umeme vya majumbani, kinachomilikiwa na Wageni kutoka India.