Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Balozi Chipeta Awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Uholanzi
Oct 20, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Mhe. Caroline Kitana Chipeta, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi.

Hafla hiyo imefanyika katika moja ya Kasri za Kifalme iliyoko Noordeinde, The Hague,  Uholanzi tarehe 19 Oktoba, 2022.

Julai 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi