Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Elimu Bure ya JPM Yaikuna Uingereza
Aug 22, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_9876" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari alipokuwa akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika na Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Rory Stewart (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na:  Bushiri Matenda na Frank Shija

Sera ya Elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini Tanzania, imeigusa Serikali ya Uingereza na hivyo kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano ulipo baina ya nchi hizo mbili.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusiana na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Jumuiya ya Madola na Idara ya Ushirikianano katika Maendeleo ya Kimataifa.

  [caption id="attachment_9877" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika na Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Rory Stewart akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipokuwa anatambulishwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) leo Jijini Dar es Salaam. Waziri huyo amekuja nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo kesho anatarjiwa kukutana na Rais Dkt. Jonh Pombe Magufuli.[/caption]

Balozi Mahiga amesema kuwa Uingereza ni ya pili miongoni mwa Wahisani wanaotoa misaada ya kimaendeleo ikiifuatia Benki ya Dunia (WB), hivyo katika mantiki ya nchi zinazotoa misaada ya kimaendeleo kwa Serikali ya Tanzania ni ya kwanza.

“Serikali ya Uingereza ni moja ya nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini katika biashara, viwanda na  sekta binafsi. Pamoja na kuwa zipo nchi nyingi zaidi tunazoshirikiana nazo kibiashara, Uingereza ni miongoni mwa nchi tano zinazowekeza zaidi nchini,” alisema Balozi Mahiga.

Aliongeza kuwa mbali na ushirikiano uliopo baina ya Serikali za nchi hizo mbili, Uingereza imeendelea kushirikiana na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGO’s), Sekta ya Afya, Elimu na mahusiano baina ya watu na watu.

[caption id="attachment_9880" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika na Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Rory Stewart akielezea jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipokuwa anatambulishwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya Bw. Salvatory Mbilinyi. Waziri huyo amekuja nchini kwa ziara ya siku mbili ambapo kesho anatarjiwa kukutana na Rais Dkt. Jonh Pombe Magufuli. (Picha na: Frank Shija).[/caption]

Akitoa shukrani kwa niaba ya Serikali Balozi Mahiga ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa misaada inayotoa katika kukabiliana na changamoto za usafirishaji haramu wa binadamu, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, ujangili na utakatishaji wa fedha.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anyeshughulikia Masuala ya Afrika, Jumuiya ya Madola na Idara ya Ushirikiano katika Maendeleo ya Kimataifa, Rory Stewart amesema kuwa amefurahi kuja Tanzania na kupata fursa ya kutembelea baadhi ya shule Jijini Dar es Salaam na pia amefurahia Sera ya Elimu bure inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Mgufuli.

Aidha Waziri Stewart amesema kuwa kufuatia kuridhishwa na Sera hiyo Serikali ya Uingereza itatoa msaada wa paundi milioni  140 za Uingereza kwa lengo la kusaidia katika sekta ya elimu ili kuboresha miundombinu muhimu katika sekta hiyo.

“ Nimeridhishwa na Sera ya Serikali ya Elimu bure, na kutokana na muitikio mkubwa wa wazazi kuwapeleka watoto shule hali inayopelekea kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanafunzi, tumeona nasi tushiriki katika kuboresha sekta hiyo.”  Alisema Waziri Stewart.

Mbali na msaada huo, Serikali ya Uingereza imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika mapambano dhidi ya majangiri, uhifadhi wa wanyamapori na mazingira ambapo ameipongeza Tanzania kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha inalinda maliasili zake.

Ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza ni wa muda mrefu na wa kihistoria na kiutamaduni kupitia matumizi ya lugha moja ya kiingereza.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi